loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba- Wachezaji wote wapimwe corona

KLABU ya Simba imeiomba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuchukua vipimo vya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa klabu zote kabla ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na mechi za ligi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mtendaji wa timu hiyo, Senzo Mazingiza alisema anaishukuru serikali kwa kuruhusu ligi ichezwe na kuomba kuchukua vipimo vya wachezaji wa timu zote kujua kama hawana ugonjwa huo.

Alisema vipimo hivyo vichukuliwe kabla ya kuanza ligi na warudie tena kwa wachezaji wote ili kupunguza au kuondoa kabisa hofu miongoni mwao.

“Pamoja na kuruhusu ligi ichezwe, bado naiomba serikali kuchukua vipimo kwa wachezaji wa timu zote na viongozi kabla ya kuanza mazoezi na ligi itakapoanza kuchezwa ili kuondoa hofu miongoni mwao,” alisema Mazingiza.

Mazingiza alisema baada ya kutolewa mwongozo kutoka serikalini wachezaji wa kikosi hicho wanatarajia kuanza mazoezi kesho kutwa kujiandaa na michezo iliyosalia.

“Tunategemea kuanza mazoezi na dhamira yetu ni kujipanga kupata ushindi ili kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), “alisema.

“Kwa sasa tunasubiri TFF na Bodi ya Ligi watupe utaratibu wa namna gani tutarejea uwanjani na tutatoa ushirikiano wa kutosha hata ikihitajika kupima afya za wachezaji wetu”.

Hivi karibuni Serikali imeruhusu Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na la Pili pamoja na Kombe la Shirikisho zitechezwe katika vituo viwili baada ya kusitishwa kwa muda kufuatia ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid-19) unaosababishwa na virusi vya corona.

Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho zitachezwa Uwanja wa Taifa, Uhuru na Azam Complex, Dar es Salaam na Ligi Daraja la Kwanza na la Pili zitachezwa jijini Mwanza kwenye viwanja wa CCM Kirumba na Nyamagana.

Hivi karibuni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema wachezaji na benchi la ufundi watakuwa wakipimwa joto la mwili kabla ya mechi.

Machi 17 baada ya Tanzania kuripoti mgonjwa wa kwanza wa COVID-19, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitangaza kusimamisha shughuli zote za michezo nchini pamoja na mikusanyiko yote na kufunga shule na vyuo kwa siku 30 kabla ya kuongeza tena

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi