loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga kumpa kazi Mshauri La liga

KLABU ya Yanga imesema wiki hii, watasaini ushirikiano wa kazi na mshauri wa La Liga, Carraca Antonio ambaye atasaidia kuwashauri juu ya njia sahihi kutekeleza mabadiliko.

Yanga wanakaribia kuanza safari ya mabadiliko ili iweze kufanya kazi kwa njia yenye faida kwa kukumbatia mfumo wa uendeshaji wa uwekezaji.

Akizungumza jana, Ofisa mwamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz alisema wakisaini mkataba, wataanza rasmi mabadiliko.

Hii inakuja baada ya klabu kufanya utafiti wa kina juu ya nani mshauri ambaye anaweza kusaidia kuiongoza timu hiyo kwenye ustawi wa kiuchumi na kuifanya kuwa moja ya klabu za ushindani kwenye barani Afrika.

“Kwa kuzingatia hili, tulimchagua La Liga kuwa mshauri, tunaamini kwamba ana sifa zinazotufanya kufika mbali kwenye mabadiliko,” alisema Nugaz.

Pia alitoa wito kwa mashabiki na wanachama kutoa ushirikiano uongozi ili ndoto za kuibadilisha Yanga zifanikiwe kwa urahisi.

“Vitu vingi vitaathiriwa tunapokwenda kwenye mabadiliko katika suala la usimamizi wa klabu, idara ya masoko na idara zingine pia.

“Wote tufanye kazi kwa kushirikiana Mwenyekiti wetu Mshindo Msolla ili tufike katika nchi iliyoahidiwa kwa urahisi na kuruhusu michakato ianze mapema,” alisema Nugaz.

Hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Msolla alianzisha agenda ya ‘Twende Kwenye Mabadiliko’ ambayo alisema kuwa ni hatua ya kwanza kufikia kilele cha mabadiliko ya klabu.

“Moja ya ahadi zangu wakati wa kipindi cha kampeni ni Yanga kuelekea mabadiliko na kuiwezesha kujiendesha kwa njia ya kisasa. Ndoto hiyo imefikiwa polepole ndio sababu tunahitaji kuwa pamoja katika mchakato mzima.

“Nimefurahi tumeanza msingi wa kufanikisha jambo hili kubwa katika historia ya klabu yetu na tutaendelea kuihabarisha familia ya Yanga kila hatua tunayofanya kupitia Azam TV na Yanga TV,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu hiyo, Hassan Bumbuli aliwahakikishia wana Yanga nchini kwamba watajumuishwa katika mchakato mzima wa mabadiliko.

“Tutakuwa tunawahabarisha kila hatua tuliyofikia kwa sasa tunangojea kusaini rasmi mkataba na mshauri wa La Liga ambaye atatusaidia katika mchakato wote wa mabadiliko.”

“Mwenyekiti alisema kuwa hivi karibuni, viongozi wa matawi kote nchini wataitwa kwa ajili ya semina ya kile tunachokusudia kufanya wakati wa mchakato wa mabadiliko ili wanaporudi kwenye maeneo yao, wanapaswa kuwaambia wanachama wao walichojifunza, “alisema.

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    Robert mwaipopo
    25/05/2020

    Tunashukuru kwa habari nzuri lkn toeni habari kwa wakati.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi