loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha - Tutakosa faida uwanja wa nyumbani

KOCHA wa Tanzania Prisons, Mohammed Rishard ‘Adolf’amesema kambi ya kikosi hicho ya kujipanga na michezo iliyosalia ya Ligi Kuu Tanzania Bara itaanzia Mkoa wa Mbeya.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Adolf alisema uongozi wa timu hiyo baada ya kupata taarifa ya michezo kuchezwa kwenye kituo kimoja walifanya kikao na kuazimia kambi ianzie Mbeya ili kupata baraka kutoka kwa wapenzi na mashabiki wao.

“Kambi yetu itaanzia mkoani Mbeya nafikiri itakuwa ya wiki moja, kabla ya kwenda Dar es Salaam, kufutia uongozi wa timu kufanya kikao baada ya kusikia taarifa ya michezo ya ligi itachezwa kwenye kituo kimoja,” alisema.

Alisema mipango yao ni kuhakikisha kwenye michezo tisa iliyosalia wanapata ushindi utakao wasaidia kujiweka kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Pia alisema bado wapo kwenye wakati mgumu kwani walikuwa na mategemeo michezo yao itafanyika kwenye uwanja wa nyumbani wa Sokoine lakini mambo yamebadilika kutokana na dharura iliyotokana na janga la ugonjwa wa corona.

“Msimu umeanza vibaya kwanza tulianza kutumia viwanja vya Samora Iringa na Jamuhuri Dodoma baada ya uwanja wetu kufungiwa na sasa tunaenda kutumia Uwanja wa Taifa hatuwezi kupata faida ya uwanja wa nyumbani,” alisema Adolf.

Aidha alisema baadhi ya mipango itakwama kutokana na kutokupata faida ya uwanja wa nyumbani lakini atawajenga wachezaji wake kisaikolojia na kiushindani kuipigania timu kupata ushindi.

Michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Azam (ASFC) itachwezwa katika Uwanja wa Uhuru, Taifa na Azam Complex baada ya serikali kuruhusu ligi kuendelea kuanzia Juni Mosi, kutokana na hali ya ugonjwa wa corona kupungua.

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi