loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Majimaji yajipanga kurudi Ligi Kuu

MENEJA wa Maji Maji FC, Shaibu Ibrahim amesema wamejipanga vyema kupambana kwa hali na mali ili kushinda mechi zake nne za Ligi Daraja la Kwanza na kurejea Ligi Kuu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Shaibu alisema ana imani kubwa na timu yao itapambana iweze kufanya vyema katika mechi watakazocheza katika kituo cha Mwanza.

‘’Tunashukuru wachezaji wetu wengi ni wa hapa Songea hivyo kuanzia leo (jana) wataanza kurejea kuendelea na maandalizi ya ligi,’’ alisema Shaibu.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu za Mbambi Vijana FC na Matalawe FC alisema mechi walizobakiza ni dhidi ya Njombe Mji FC, Dodoma Jiji FC, African Lyon na Pan African.

Pia aliwaomba wadau na wapenzi wa soka mkoani Ruvuma kuendelea kuisaidia timu yao misaada mbalimbali ikiwemo chakula, maji pamoja na fedha ili wachezaji waweze kujikimu watakapokuwa kwenye ligi mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa timu hiyo, Peter Mhina alisema timu itaanza mazoezi leo kuhakikisha inafanya vyema katika michezo hiyo.

Katika msimamo wa kundi A, Maji Maji FC ipo katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 34 baada ya kucheza michezo 18, ikiwa imefunga mabao 20 na kufungwa mabao 14.

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi