loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NBA kuanza msimu Julai

NBA iko kwenye mazungumzo ya kuanza tena msimu kwenye hoteli ya Disney, Florida, mwishoni mwa Julai. Msimu ulisimama Machi 11 kwa sababu ya janga la virusi vya corona.

Inatarajiwa Disney, ESPN Wide World of Sports Complex inaweza kuwa sehemu moja ya michezo, mazoezi na makazi.

Ligi hiyo ipo katika mazungumzo na Chama cha taifa cha wachezaji kulingana na msemaji wa NBA, Mike Bass.

“Kipaumbele chetu kinaendelea kuwa afya na usalama wa wote wanaohusika, na tunafanya kazi na wataalamu wa afya ya umma na viongozi wa serikali juu ya miongozo kamili ili kuhakikisha itifaki na usalama wa matibabu unapatikana,” alisema Bass.

Msimu wa kawaida bado haujakamilika. Timu ya Milwaukee Bucks inaongoza kanda ya Mashariki na Los Angeles Lakers iko juu katika kanda ya Magharibi.

Hadi jana kwa mujubu wa mtandao wa corona. tuply. co.za, watu 1.669, 311 wamethibitishwa kuugua virusi vya corona nchini humo na vifo vikiwa vimefikia 98,740.

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes ...

foto
Mwandishi: FLORDA, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi