loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mchezaji Bournemouth akutwa na corona

MCHEZAJI wa timu ya Bournemouth ambaye jina lake halikutajwa ni moja kati ya watu wawili waliogundulika kuwa na virusi vya corona na kufanya idadi wanaougua kufi kia nane sasa.

Hata hivyo, utambulisho wa mchezaji huyo umefichwa na sasa watajitenga kwa siku saba. Uchunguzi ulifanyika Jumanne, Alhamisi na Ijumaa ya wiki iliyopita, wachezaji 996 na wafanyakazi wa klabu mbalimbali nchini humo tayari wamepimwa.

“Kufuatia kanuni madhubuti za kurudi kwa Ligi Kuu, uwanja wa mazoezi wa klabu unabaki kuwa mazingira salama ya kufanya kazi kwa wachezaji na wafanyikazi wengine, ambao wataendelea kupimwa Covid-19 mara mbili kwa wiki,” ilisema taarifa ya Bournemouth.

Matokeo ya raundi ya kwanza, yaliyotangazwa Mei 19, yalikuwa ya watu sita kutoka kwenye klabu tatu na wahusika waliopimwa ni 788. Idadi hiyo ni pamoja na vipimo vya meneja wa Watford, Adrian Mariappa na meneja msaidizi wa Burnley, Ian Woan ambao waligundulika kuwa na corona.

Kwa mzunguko wa pili, idadi ya vipimo inayopatikana kwa kila klabu iliongezeka kutoka 40 hadi 50. Timu zimeanza mazoezi yasiyokuwa ya kugusana tangu Jumanne kwa mara ya kwanza tangu Ligi Kuu kusitishwa Machi 13 kwa sababu ya janga la corona, na zimesalia mechi 92 msimu kumalizika.

Wakizungumza Ijumaa, Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu, Richard Masters alisema kwa kujiamini kuwa ligi hiyo itaanza tena mwezi Juni.

Bundesliga ya Ujerumani tayari ilishaanza tena, wakati Jumamosi Waziri Mkuu wa Hispania alisema La Liga inaweza kuanza Juni 8 bila mashabiki.

Nahodha wa Watford, Troy Deeney na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Ian Wright ni miongoni mwa waliowauliza maofisa wa serikali kuhusu hatari ambayo inaweza kutokea kwa wachezaji wenye asili ya Afrika, Asia na watu wa pembezoni.

Ofisi ya Takwimu za Kitaifa inasema wanaume na wanawake weusi wana uwezekano wa kufa mara mbili kwa corona kama watu weupe huko England na Wales.

Mshambuliaji Deeney na kiungo wa Chelsea, N’Golo Kante alisema hawezi kufanya mazoezi ya pamoja wiki iliyopita kwa kuhofia kuambukizwa virusi vya corona.

Katika mkutano wa ‘online’ wa kuelezana ukweli na uwazi, wataalamu wa matibabu, pamoja na Naibu Mkuu wa Matibabu, Jonathan Van-Tam, waliulizwa namna ya kumaliza hatari.

Deeney na Wright, ambao pia walijumuika kwenye jukwaa la ‘Online’ na mshambuliaji wa zamani wa Newcastle, Shola Ameobi na Mkurugenzi wa zamani wa ufundi wa Chelsea, Michael Emenalo, waliambiwa kuwa hatari ya watoto wachanga na wachezaji kuambukizwa ni kidogo.

Lakini wasiwasi pia uliibuka juu ya kupeleka maambukizo kwa familia. Jumuiya ya Wataalamu wa Mpira wa Miguu, ambayo pia ilikuwa katika mahudhurio, imeomba utafiti zaidi kufanywakatika suala hilo.

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi