loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Babu Njenje azikwa Kisutu

MWANAMUZIKI mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro ‘Wana Njenje’, Mabrouk Hamis Omar ‘Babu Njenje’ (pichani) amefariki dunia jana alfajiri jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu na kuzikwa jana katika makaburi ya Kisutu.

Akizungumza Dar es Salam jana, mmoja wanamuziki wa bendi hiyo, John Kitime alisema ni kweli Babu Njenje amefariki dunia na msiba upo nyumbani kwake Mtaa wa Mindu Upanga.

“Ni kweli Babu Njenje amefariki, naelekea msibani nyumbani kwake Mtaa wa Mindu, Upanga ambapo taratibu za mazishi zitafanyika,” alisema.

Mkongwe huyo ambaye alipata kiharusi kwa miaka mitano sasa, ameacha mke na watoto wawili.

Babu Njenje mwenye umri wa miaka 73 atakumbukwa kwa nyimbo zake kama Njenje, Kinyaunyau, Boko, Ndembele, na nyingine nyingi.

Kilimanjaro bendi hutumbuiza kila Jumamosi pale daraja la Selander ikiwa na wanamuziki wakongwe akiwemo Nyota Waziri, Asma Makau, Shadee, Kitime.

Babu Njenje amekuwa na bendi hiyo kwa miaka 47 tangu inaanzishwa na jina la Njenje lilitokana na wimbo uliokuwa ukiitwa Njenje aliowahi kuuimba.

Katika hatua nyingine, Chama cha Muziki wa Dansi, (Chamudata) kimetuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanamuziki wote wa dansi kwa kuondokewa na mpendwa wao.

“Kifo cha Babu Njenje ni pigo kwa muziki wa dansi na ameacha alama katika dansi, tumwombee apumzike salama,” alisema Hassan Msumari, Katibu wa Chamudata.

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    CLEOPHACE.M.COSTANTINE
    25/05/2020

    WANA MZIKI WA DANS POLENI WOTE NAOMBA MUIGE MAZURI ALIYOFANYA.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi