loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kampuni yawezesha kuuza, kununua kuepuka corona

ILI kukabiliana na ugonjwa wa Covid- 19 unaosababishwa na virusi vya Corona, Kampuni ya Kupatana imeimarisha jukwaa la kuhakikisha Watanzania wanafanya biashara kununua na kuuza bila mikusanyiko.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kupatana.com, Philip Ebbersten ilisema hatua hiyo ni kutoa fursa kutumia jukwaa hilo kufanya biashara wakati huu wa kupambana na ugonjwa wa Covid-19.

Alisema malengo na mwelekeo wa Kupatana ni kuwa na wateja wenye mafanikio kuongeza biashara.

“Kwa sasa tukiwa na janga la Covid-19 ni muhimu watu na biashara zao ziendelee wakiwa mbali na mikusanyiko ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo. Kupatana ndio pa kukupa fursa hiyo,” alisema.

Ebbersten alisema kurahisisha ufanyaji biashara, Kupatana imeunganisha shughuli na huduma za M-Pesa.

“Kupatana inatangaza M-Pesa imeunganishwa kama njia ya malipo katika jukwaa hili. Watumiaji wote wa M-Pesa watakuwa na uwezo wa moja kwa moja na kwa urahisi kujiunga na kutumia huduma ya Premium Ads, mteja anayelipia, utakuwa na uwezo wa kutumia huduma zote za matangazo ya Premium Ads. Hii inasaidia kujiwekea nafasi kubwa zaidi ya kuuza bidhaa zako kwa haraka na kwa uhakika.

“Sasa watumiaji wa mtandao wa simu wa Vodacom watakuwa sehemu ya jukwaa kubwa la biashara.

"Tunayo furaha ya kuunganisha huduma zetu na huduma za Vodacom MPesa,” alisema Ebbersten. Ebbersten alisema taasisi yake pia imepunguza ada ya matangazo na kutoa punguzo kwa asilimia 80.

“Vilevile, wakati ambapo tunazindua huduma za malipo kwa M-Pesa, pia tunapunguza ada kwa wateja wa matangazo ya Premium. Hii ni ofa maalum katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid-19 ambayo inalenga kuhamasisha biashara ya masafa ili kuepuka misongamano. Tunatumaini kwa kufanya hivi tutashiriki katika kuzuia kuenea kwa virusi huku tukichangia katika kuendeleza biashara,” alisema.

Alisema kuanzia jana Kupatana inatoa punguzo la asilimia 80 kwa matangazo ya Premium yawe nafuu zaidi kwa kila mtu na matangazo yote ya Premium yanaweza kurejeshwa juu kwa gharama ndogo zaidi.

“Unaweza kupata punguzo la ziada la asilimia 10 iwapo utapata "hati punguzo" kutoka mojawapo ya mawakala wetu. Matangazo ya bure yataendelea kuwepo kwa wiki moja pekee. Tunaamini kwa mfumo huu tutawahudumia wauzaji na wanunuzi kwa usawa,” alisema.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi