loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mawaziri SADC watathimini usalama wa chakula

MAWAZIRI wa Sekta wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi wa nchi zilizo Kusini Mwa Jangwa la Sahara (SADC) wamekubaliana kufanya tathimini ya miezi mitatu ya usalama wa chakula kwa kuzingatia mazingira ya sasa ya kuwepo kwa majanga ukiwemo ugonjwa wa COVID-19.

Uamuzi huo umefanyika katika mkutano wa mawaziri uliofanyika mwishoni mwa wiki chini ya uenyekiti wa Luhaga Mpina ambaye ni Waziri wa mifugo na Uvuvi nchini Tanzania.

Mkutano huo uliofanyika kwa mtandao na kuhudhuriwa na mawaziri 11 Kati ya 16 wa sekta ya kilimo, Mifugo na Uvuvi Sadc , ulilenga kuangalia namna ya kuimarisha sekta hizo kuchangia maendeleo ya uchumi.Mpina alisema baada ya tathimini, wataangalia nchi zenye changamoto na kuangalia kuziondoa .

"Kuna wenzetu kwa sasa wamejifungia kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19, tulikubaliana baada ya miezi mitatu kila nchi ieleze changamoto inayowakabili ili tuweze kusaidiana," alisema Mpina.

Mpina alisema nchi ambazo hazina bahari na maziwa zimeazimia kuanzisha ufugaji wa viumbe maji ili kwenda na kasi ya upatikanaji vitoweo na kuimarisha afya za wananchi kwa nchi wanachama wa SADC.

Aidha Mpina alisema pia baadhi ya changamoto zitatatuliwa na nchi husika na changamoto nyingine watasaidiana kuzitatua kama nchi wanachama.

Mpina alisema Mwenyekiti wa SADC, Rais John Pombe Magufuli yuko bega kwa bega kuhakikisha vikao vyote vinafanyika licha ya kuwepo Corona kwa kutumia ushauri wa mawaziri wa afya kufanya kwa kutumia mawasiliano ya video

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi