loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

'Watanzania waendelee kuomba Mungu amalize corona'

WATANZANIA wametakiwa kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu aondoe ugonjwa wa homa kali ya mapafu Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

Wito huo umetolewa na Ustaadh Maulid Harun wa Taasisi ya Ansaar Muslim kwenye hotuba ya swala ya Idd El Fitr iliyoswaliwa jana jijini hapa katika viwanja vya wazi.

Aliwataka Waislam wazingatie hilo. Alisisitiza kuwa njia ya kujinasua ni kumrudia Mwenyezi Mungu kwa kuomba dua ili waondokane na ugonjwa huo kwani hata nchi zilizoendelea kiteknolojia pia zimekwama na kuamua kumrudia Mungu.

Tanzania imefanya maombi maalum ya siku tatu ya kumshukuru Mungu kwa kupunguza ugonjwa huo.

“Dunia nzima sasa inalia na Corona, hata nchi zilizoendelea pamoja na kuwa na teknolojia ya hali ya juu na utajiri pia zimeshindwa na zimemrudia Mungu asaidie, lazima tumwombe Mwenyezi Mungu atuepushe na maradhi haya pamoja na kuchukua tahadhari kwa kufuata ushauri wa wataalam wa afya,” alisema.

Aliwataka Waislamu kuendelea kufanya matendo mema kama waliyoyafanya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kuzidisha ibada na matendo mema na kuonya watu kutokuitumia Sikukuu ya Idd kufanya maasi kwani itakuwa haina maana kwao kufunga na kuomba toba halafu wanarudia matendo machafu.

“Tujitahidi tusimame kwa Mwenyezi Mungu kwa kufanya ibada miezi mingine kama tulivyofanya kwenye mwezi wa Ramadhani kutokana na kuwa ibada haina kikomo kila siku Mungu yupo,” alisema.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Tanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi