loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakurugenzi kizimbani hasara ya bil 3.5/-

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya Mirerani katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Manyara kwa kosa la uhujumu uchumi wakidaiwa kulisababishia taifa hasara ya zaidi ya Sh bilioni 3.5.

Wakurugenzi hao na wafanyakazi wawili, mlinzi na mhandisi wa mgodi huo walifikishwa mahakamani mara ya kwanza na kusomewa mashtaka ya kesi ya uhujumu uchumi ambapo hawakutakiwa kujibu lolote.

Wakisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa, Simon Kobelo, Mwendesha Mashtaka ambaye pia ni Wakili wa Serikali, Tarsila Asenga aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Hussein Gonga, Faisali Shabai, Abubakari Lombe na Anthony Maswi.

Asenga alidai waliisababishia serikali hasara ya Sh 3,558,086,418.80 kwa kuongoza genge la uhalifu, kushindwa kufuata amri halali za mkaguzi wa madini na kukaidi amri halali, kushindwa kufuata kanuni za usalama za madini, kukwepa kodi, kusababishia hasara mamlaka za serikali na utakatishaji fedha.

Asenga alidai mtuhumiwa Abubakari Lombe alitenda kosa akiwa Mlinzi Mkuu wa kampuni hiyo wakati Anthony Maswi alifanya akiwa ni mhandisi kabla ya mgodi huo kumilikiwa na serikali Desemba 2019.

Amedai watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda makosa hayo saba wakati wakiwa katika mgodi wa CFT ambao uko katika mgodi wa Tanzanite One Mining Ltd kwa kumwaga maji chini ya mgodi huo kuzuia uchimbaji usifanyike kwa wachimbaji wengine kitendo ambacho kilitajwa kuwa sio utaratibu kisheria.

Watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa sasa hadi jalada hilo litakaporudi kutoka kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu (DPP). Walipelekwa rumande kwa kesi kutokuwa na dhamana na kwamba kesi hiyo itatajwa tena Juni 22, 2020.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Theddy Challe, Babati

1 Comments

  • avatar
    CLEOPHACE M COSTANTINE
    25/05/2020

    SHERIA ITOE ADHABU SITAHIKI.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi