loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Suluhu mgororo wa madereva imeonesha ujirani wa kweli

KUIBUKA kwa ugonjwa wa COVID-19 katika nchi mbalimbali duniani kumesababisha magonjwa, vifo na changamoto mbalimbali za kiuchumi.

Pia, ugonjwa huo umekuwa chanzo cha migogoro ya nchi mbalimbali zinapopambana kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika mapambano ya vita yoyote, zinahitajika hekima na busara na ndio hivyo hivyo katika vita ya kuukabili ugonjwa huo, ambapo baadhi ya nchi zimefanya maamuzi ya kufunga mipaka, kuweka zuio na kupima raia wake na wageni wanaoingia mipakani. Lemgo la hatua zote hizo ni kuwalinda wananchi kuhakikisha kuwa wanakuwa salama.

Katika wiki za karibuni Tanzania imekabiliwa na changamoto katika mipaka yake na nchi jirani, ikiwemo Rwanda, Kenya na Zambia, hali iliyosababisha msongamano ya malori, yanayobeba bidhaa mbalimbali kupeleka katika nchi hizo.

Kutokana na changamoto hizo, wapo waliofikiri sasa nchi hizo jirani zitaingia katika migogoro mikubwa na wakati mwingine kutokuwa na mwingiliano wa watu, bidhaa na masuala mengine ya kidiplomasia.

Lakini, hali imekuwa tofauti, kutokana na tofauti hizo kumalizwa kwa busara na safari kuendelea. Changamoto kubwa kwa maderava, imekuwa suala la upimaji wa virusi vya corona.

Wakati fulani kulikuwa na madai kuwa madereva wa Tanzania, wanasambaza virusi hivyo katika nchi mbalimbali, jambo ambalo si kweli, baada ya kufuatiliwa kwa undani na mamlaka husika.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri na marais wa nchi husika, waliingilia kati na kufanya mazungumzo, ili kuhakikisha suala hilo linatatuliwa bila kukandamiza upande wowote.

Changamoto ilianzia mpaka wa Tanzania na Rwanda, baada ya serikali ya Rwanda kutoa agizo la madereva wa Tanzania kuishia mpaka wa Rusumo na kukabidhi bidhaa na mizigo kwa madereva wa Rwanda, ili kuipeleka nchi mwao. Hatua hiyo ilipingwa vikali na wamiliki wa malori wa Tanzania.

Katika kumaliza changamoto hiyo, mawaziri wa Uchukuzi wa nchi hizo mbili, walikaa na kufikia muafaka, kwa kila dereva kupimwa anapoingia katika pande za nchi zote mbili na amani ikarejea.

Siku kadhaa baadaye, ukaibuka mgogoro wa madereva malori baina ya Kenya na Tanzania, lakini ufumbuzi ulipatikana, baada ya watendaji wa ngazi mbalimbali wa serikali za Tanzania na Kenya, kukutana mpakani eneo la Namanga.

Katika kikao hicho kilichoshirikisha mawaziri, wakuu wa mikoa na wataalam wa sekta mbalimbali, viongozi hao walikubaliana kuanzia sasa madereva wa malori, watapimwa katika nchi zao na kupewa cheti, kitakachotambulika popote watakapokwenda kwa muda wa siku 14.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Issack Kamwelwe na Waziri wa Usafirishaji wa Kenya, James Macharia walisaini mkataba wa makubaliano, wakieleza kufikia makubaliano kuhakikisha biashara zinaendelea na pia tahadhari za kukabiliana na corona zinaendelea kuchukuliwa.

Kumalizika kwa mgororo huo, kulifanyika baada ya Rais Dk John Magufuli kufanya mazungumzo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kukubaliana watendaji kumaliza tofauti zilizopo.

KATIKA miaka ya karibuni msimu wa mavuno kumekuwa na watu ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi