loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wachezaji Yanga kupimwa corona

WACHEZAJI wa Yanga leo wataanza kupimwa afya zao, ikiwemo corona tayari kuanza mazoezi Juni Mosi kwa ajili ya kujiandaa na mechi zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Rais Dk. Pombe Magufuli wiki iliyopita alitangaza kurejea kwa shughuli zote za michezo kuanzia Juni Mosi, na vikao vimekuwa vikiendelea, na Ligi Kuu Tanzania Bara imepangwa itachezwa katika kituo kimoja cha Dar es Salaam kwenye viwanja vya Taifa, Uhuru na Chamazi.

Msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema jana kuwa, wachezaji wote wa timu hiyo leo watafanyiwa vipimo kwenye uwanja wao wa mazoezi uliopo katika Shule ya Sheria Tanzania eneo la Mawasiliano, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Bumbuli alibainisha kuwa wachezaji hao watapimwa malaria, sukari, uzito pamoja na corona ili kujua afya zao kabla ya kuanza rasmi mazoezi Juni Mosi na baadae Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Kesho (leo) wachezaji wetu wote tutawafanyia vipimo vya malaria, sukari, uzito na corona ili kujua hali zao pale katika uwanja wetu wa mazoezi na wale watakaokuwa na matatizo watapewa ushauri, “alisema Bumbuli.

Akizungumzia suala la kurejea kwa Kocha Mkuu, Luc Eymae aliyekwama kwao Ubelgiji alisema hajui atarudi lini pamoja na wasaidizi wake waliopo Afrika Kusini baada ya baadhi ya nchi kuendelea kuwa na zuio la anga.

Alisema baadhi ya nchi bado anga zao zimeendelea kufungwa, hivyo hawajui makocha hao watarudi lini, lakini mara mambo yatakavyokuwa tayari watarejea nchini kujiunga na timu hiyo, ambayo sasa itakuwa chini ya Boniface Mkwasa.

Wakati ligi hiyo na michezo mingine ikisimamishwa Machi, Yanga walikuwa na pointi 51 baada ya kucheza mechi 27 wakiwa nyuma ya vinara Simba wenye pointi 71 na Azam FC iliyopo katika nafasi ya pili yenye pointi 54 zote zikiwa zimeshuka dimbani mara 28.

Namungo FC ya Lindi iko katika nafasi ya nne ikicheza mara 28 na kujikusanyia pointi 50 huku Coastal Union ya Tanga ikicheza mara 28 na kujipatia jumla ya pointi 46 katika mbio hizo za kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa mwaka 2019/2020.

MKOA wa Pwani umeanza kwa kishindo maandalizi ya kushiriki mashindano ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    Amosi jumanne
    26/05/2020

    0689093954

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi