loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwalusako kuzikwa Mbeya

MWANASOKA wazamani wa Yanga, Pan African na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Lawrence Mwalusako amefariki dunia jana na anatazamiwa kuzikwa Mbeya Alhamisi.

Mwalusaka aliyefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha MOI, mwili wake utasafirishwa kesho Jumatano kwenda Kyela, tayari kwa mazishi siku inayofuata.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Soka Tanzania (Spotanza), Mussa Kisoki alisema jana kuwa mchezaji huyo aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga alifariki jana asubuhi katika hospitali hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa.

Akielezea ratiba ya safari ya mwisho ya Mwalusako itakavyokuwa, Kisoki alisema kuwa baada ya mwili huo jana kulala nyumbani kwake Ubungu, leo kuanzia saa 4 asubuhi utaombewa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Ubungo na baadae utalazwa Muhimbili kabla ya kusafirishwa kesho.

Alisema wadau wa soka wamepata pigo kubwa, kwani Mwalusaka hata alipostaafu mchezo huo, aliendelea kucheza soka katika timu ya maveterani na hakupenda kabisa mtu kuleta utani katika soka.

Raha ya milele umpe eeh bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa Amani, Amina.

MKOA wa Pwani umeanza kwa kishindo maandalizi ya kushiriki mashindano ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi