loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ligi Kuu Burundi kumalizika Juni 28

LIGI Kuu Burundi inaendelea, huku ikitarajiwa kukamilika Juni 28, imeelezwa. Hadi sasa, Burundi ndio nchi pekee ya Afrika kuendelea kucheza soka wakati huu wa mlipuko wa janga la virusi vya corona, huku ligi hiyo ikielekea katika hatua muhimu.

Musongati FC ilitoka sare ya kufungana mabao 3-3 na Athletico Academy katika mechi zilizofanyika katikati ya wiki na kupunguza tofauti yake na vinara Le Messager Ngozi hadi kufikia tatu wakati zimebaki raundi tatu kabla ligi hiyo haijamalizika.

Ngozi inasaka taji lake la pili wakati Musongati ikipambana kutwaa taji la kwanza, na zote kila moja ikibakisha mechi mbili za nyumbani na moja ugenini kabla ya kukamilika kwa msimu wa ligi hiyo. Wakati ligi kubwa zote za soka zikiwa zimesimama katika nchi zingine za Afrika au zimefutwa kutokana na mlipuko wa Covid-19, Burundi iliamua kuendelea kucheza.

Watazamaji ambao walishuhudia Musongati ikiacha pointi mbili baada ya kupata bao la dakika za mwisho dhidi ya Athletico katika mji mkuu wa Gitega, wengi hawakuzingatia baadhi ya tahadhari ya virusi vya corona. Joto la kila mtazamaji aliyeingia kwenye uwanja huo unaochukua watu 10,000 wa Stade Ingoma liliangaliwa na kupakwa vitakasa mikononi mwao.

Lakini hakukuwa na suala la watu kukaa mbalimbali majukwaani, huku mashabiki hao wakikaribiana sana. Wachezaji wengi walipuuza maagizo yaliyopita, ambayo yaliwataka kutokumbatiana na kushikana mikono na wachezaji wenzao wakati wakishangilia magoli.

"Baada ya kuwasiliana na waziri wa afya, uamuzi uliofikiwa ni kuendelea na mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza na Pili, “alisema msemaji wa shirikisho hilo la soka.

Nchi zingine zilizoamua kuendelea na ligi za nyumbani wakati COVID-19 ikichukua uhai wa maelfu ya maisha ya watu duniani kote ni pamoja na Belarus, Nicaragua na Tajikistan.

Mechi iliyofanyika hapa, mji ambao umechukua nafasi ya Bujumbura kama mji mkuu, una watu wengi na soka limerejea baada ya kumalizika kwa mapumziko ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Mamilioni ya Warundi Jumatano walifurika katika vituo mbalimbali vya kupigia kura kumchagua mtu, ambaye atachukua nafasi ya Pierre Nkurunziza kama rais, na kuwachagua wabunge na madiwani.

Mbali na ratiba ya ligi Mei 30/31 na Juni June 20/21 na 27-28, Burundi pina inatarajia kukamilisha mashindano ya Kombe la FA, ambayo sasa yako katika hatua ya nusu fainali.

Washindi wa Ligi Kuu na Kombe la FA watafuzu kwa msimu wa 2020/21 wa michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika na Kombe la Shirikisho, ambayo yamepangwa kuanza Agosti 7.

Timu ya Vital’o ndio imewahi kufika mbali zaidi kwa timu za Burundi katika mashindano ya Caf wakati mwaka 1992 ilipocheza fainali ya mashindano, ambayo sasa yanaitwa Kombe la Shirikisho. Vital'O ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Africa Sports ya Ivory Coast katika mchezo wa kwanza na ilifungwa mabao 4-0 ilipochea ugenini Abidjan.

MKOA wa Pwani umeanza kwa kishindo maandalizi ya kushiriki mashindano ...

foto
Mwandishi: GITEGA, Burundi

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi