loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali kutoa mwongozo kurudi michezo

SERIKALI baada ya kufanya kikao na wadau wa michezo imesema kesho inatarajia kutoa muongozo kwa kushughuli zote za michezo, ikiwemo ile ya Ligi Kuu na mingine itakavyofanyika bila kuathiri kanuni za afya.

Muongozo huo utatolewa baada ya shughuli zote za michezo kuruhusiwa kufanyika baada ya kusimamishwa kwa takribani miezi miwili kuanzia Machi 17 kupisha janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona kufuatia kuripotiwa kuingia nchini.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo (BMT) Dk Yussuph Singo, alisema muongozo huo ni wa michezo yote na utajumuisha masuala ya kiafya utatolewa baada ya kufanya kikao kilichojumuisha Wizara ya Afya na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Tumeshafanya kikao ambacho kimetengeneza muongozo, ambao umejumuisha masuala ya afya na mambo ya kiufundi ya michezo, tumeshakamilisha tunasubiria muongozo upitiwe kwenye mchakato wa kawaida na baada ya hapo utapitiwa na wakuwa wa wizara zote mbili na kutolewa siku ya Jumatano (kesho),”alisema.

Alisema wataanza kutoa muongozo wa jumla kwa michezo yote na baada ya hapo wataanza kutoa kwa kila mchezo ili kuhakikisha kila upande mchezo unafanyika na kuzingatia tahadhari stahiki za kujikinga na janga la virusi vya corona.

Alisema kwenye kikao hicho waliwashirikisha pia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi kama ili kupata maoni yao kwakuwa mchezo wa mpira wa miguu una mambo mengi, ikiwemo kuhusisha idadi kubwa ya mashabiki.

“TFF tuliwaita pamoja na Bodi ya Ligi kwakuwa mpira wa miguu una mambo mengi kwanza kuna mechi zimebaki, pili unakusanya idadi ya mashabiki wengi uwanjani, “alisema Singo.

Muongozo huo unatarajiwa kutolewa baada ya Rais Dk John Magufuli kuruhusu shughuli zote za michezo kuendelea kuanzia Juni Mosi kwa kuwa ni sehemi ya burudani na utasaidia kuondoa hofu kwa baadhi ya watu dhidi ya ugonjwa wa corona.

MKOA wa Pwani umeanza kwa kishindo maandalizi ya kushiriki mashindano ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi