loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanaotoza 1,000/- mfuko wa mawe kukamatwa

SERIKALI imepiga marufuku kukusanya ushuru wowote ambao unapingana na sheria za madini , kanuni na taratibu zilizowekwa na wizara hiyo na kutaka wale wote watakoendfa kinyume kukamatwa na kushitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Madini Dotto Biteko alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo katika kijiji ncha Isanga, kata ya Lusu wilaya ya Nzega mkoani Tabora jana .

Alisema kwamba kuwatoza ushuru wa Sh 1,000 kwa kila mfuko wa mawe ni kosa kisheria na yeyote anayefanya hivyo anastahili kukamatwa na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi na kuwa wenye leseni kuwatoza ushuru kupitia mfuko wa mawe kila siku ni uonevyo mkubwa na katu serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hilo.

“Watu wanaofanya hivyo eti kwa lengo la kuwatambua wapasua mawe ni uonevu usiovumilika kabisa na kama unataka kumtambua mtu basi wanaweza kutambua kwa sura kwani kila siku mtu huyo yupo hapo hapo Isanga na anapasua mawe kwa ajili ya kujipatia kipato jambo hilo liwe mwisho vinginevyo mkono wa sheria utafanya kazi yake,” alisema Biteko.

Hata hivyo aliwataka wenye leseni za madini nchini kuhakikisha ushuru wowote watakaotoza uthibitiwe na ofisa madini mkazi au kutoka ofisi hiyo ili kupunguza malalamiko ya aina hiyo.

Waziri huyo wa madini aliendelea kusisitiza kuwa serikali inapenda wananchi wake wanufaike kutokana na rasilimali za nchi yao na sio watu wachache ndio wanufaike nayo.

Kabla ya kutoa kauli hiyo, wachimbaji hao walimlalamikia waziri huyo kuwa wamekuwa wakitozwa ushuru kwa kila mfuko wa mawe kiasi cha Sh 1000 .

BENKI za NIC Tanzania na CBA ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi