loader
Dstv Habarileo  Mobile
Shirika linavyosaidia jamii kukabili umasikini

Shirika linavyosaidia jamii kukabili umasikini

AWAMU ya Kwanza ya Serikali ya Tanzania iliyoongozwa na Mwalimu Julius Nyerere ilitangaza vita dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, umasikini na maradhi. ili taifa lipige hatua, taifa lilipaswa kuhakikisha jamii inajinasua dhidi ya maadui hao ili kupata ya maendeleo ya mtu binafsi, na taifa kwa jumla.

Umasikini uliloelezwa kama moja ya maadui wanaodhoofisha jitihada za maendeleo ya kada mbalimbali, ulihitaji kupambaniwa kwa ngazi mbalimbali kuanzia taifa hadi ndani ya jamii, kwa makundi na hata kwa mtu mmoja mmoja.

Serikali ilitambua ukubwa wa vita hii kwa kuitaka jamii kushirikisha kila kada kuhakikisha umasikini anatokomezwa kwa vita iliyohitaji ushirikiano.

Mwitikio wa vita hii ulianza kupiganwa kwa hatua mbalimbali, hata kuhusisha asasi na makundi yaliyoweza kuungana na serikali kuhakikisha umasikini unapigwa vita kwa vitendo.

Kutokana na hali hiyo, asasi nyingi hata sasa zimeendelea kuunga mkono serikali kwa nyakati, matukio na namna mbalimbali kuushinda umasikini.

Shirika la Kifamilia kwa Amani ya Dunia (FFWP) ni miongoni mwa asasi zilizojikita katika kupigana vita hii kwa njia ya kuisaidia jamii. Shirika hili limejikita kusaidia jamii iliyohitaji msaada kwa kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana, hivyo wanaitikia mwito wa vita hii.

Shirika hili ambalo hapa nchini makao yake yapo Kinyerezi wilayani Ilala, Dar es Salaam limekuwa likitoa elimu ya maadili kwa wanafamilia kuanzia malezi ya watoto, uhusiano mwema kwa wanandoa na wajibu wa wazazi kwa watoto.

Pamoja na wajibu wake wa kutoa elimu kwa familia, Shirika hili pia limekuwa likitoa misaada mbalimbali katika maeneo kadhaa, zikiwemo huduma za kijamii.

Akizungumza na maofisa wa Kituo cha Habari dhidi ya Umasikini (MeCAP) waliotembelea ofisini kwake, Mkurugenzi wa FFWP nchini, Stylos Simbabwene anasema shirika limesaidia katika baadhi ya huduma za jamii ili kusaidia jamii katika vita dhidi ya umasikini kwa vitendo.

Baadhi ya maeneo ambayo Shirika hilo limesaidia kwa mujibu wa Simbamwene ni pamoja na uwekaji wa mfumo wa maji safi na ukarabati wa kisima cha maji katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Dar es Salaam.

Katika kituo hicho, FFWP pia wamegharamia uwekaji wa umeme katika jengo la Dawati la Jinsia ili kuliwezesha kuhudumia wananchi wakati wote katika mazingira mazuri zaidi.

Anasema: “Pia, tumekarabati vituo vya polisi vidogo vya Manzese na Kigogo Luhanga jijini Dar.”

Simbamwene amesema Shirika lake pia limekarabati kisima cha maji katika Shule ya Msingi Mjimpya wilayani Ilala; na kukarabati wa lifti kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Tumefanya pia ujenzi wa jengo la Serikali ya Mtaa wa Msigani wilayani Ubungo, Dar es Salaam, lakini pia wilayani Temeke tumechangia vifaa katika ujenzi wa Ofisi ya CCM Azimio,” anasema Simbamwene na kuongeza kuwa, shirika limetoa misaada hata katika mikoa mingine.

“Tunafanya kazi zetu nchi nzima. Tumechangia ujenzi wa zahanati ya Engutoto iliyopo Arumeru mkoani Arusha, lakini pia uchimbaji wa visima wilayani humo,” anasema Simbamwene.

Anaongeza; “Huko Mvomero mkoani Morogoro, Shirika limejenga zahanati, kuchimba kisima cha maji na kununua gari la wagonjwa katika Kijiji cha Manza”. Mkoani Mbeya, amesema wamechimba kisima cha maji katika Shule ya Msingi Mwaheki.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/37f85da6ad2571bb684a41e8e9f8471a.jpg

Mteja anayetaka kutuma mzigo nje au kupitishia ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi