loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pemba wapongezwa kukabili corona

WANANCHI wa kisiwa cha Pemba  visiwani Zanzibar wamepongezwa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu ya Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona kwa kupunguza maambukizi yake kwa kiwango kikubwa.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Shamata Khamis Shaame akipokea vifaa vya kupambana na ugonjwa wa huo kwa hospitali nne za kisiwa cha Pemba.

Alisema mafanikio hayo yamepatikana baada ya wananchi kutekeleza masharti ya kupambana na ugonjwa huo kwa kuvaa barakoa na kupunguza mikusanyiko watu kutoka Tanga na Mombasa, Kenya wakipimwa afya zao.

''Tumepunguza maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa sababu wananchi wamekuwa watiifu wakifuata masharti ya ugonjwa huo ambayo ni kupunguza mikusanyiko isiyokuwa na lazima,'' alisema.

Aliipongeza Taasisi ya Milele kwa kushirikiana na Wazanzibari waliopo nje ya nchi kusaidia vifaa hivyo katika hospitali nne muhimu za kisiwa hicho. Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na taasisi hiyo ni pamoja na nguo maalumu kwa ajili ya watu wanaotoa huduma kwa wagonjwa wa covid-19, vifaa vya kupima joto la mwili na vitakasa mikono na sabuni.

Mratibu wa Taasisi ya Milele Pemba, Abdalla Said alisema wameamua kutoa vifaa hivyo kwa hospitali nne za kisiwa cha Pemba ikiwa ni sehemu ya kupambana na maambukizi yanayoweza kujitokeza.

Alisema wamefarijika kiasi kikubwa kuona wananchi wengi wa kisiwa cha Pemba wamehamasika ikiwemo kuvaa barakoa maeneo yote ya miji mitatu mikuu ikiwemo Chakechake, Mkoani na Wete.

''Vifaa vilivyotolewa na taasisi hiyo, lengo lake ni kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa covid-19 na kuona wananchi wako salama huku wakifanya shughuli zao za maendeleo na ujenzi wa taifa,'' alisema.

Vifaa vilivyotolewa ni vya Sh milioni 30 baadhi vimetolewa na Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi.

Akipokea vifaa hivyo, Ofisa mdhamini Wizara ya Afya Pemba, Shadya Shaaban Seif alisema msaada huo umekuja wakati muafaka Wizara ya Afya ikiongoza vita ya Covid-19 inayosababishwa na virusi vya corona.

Seif aliwapongeza wananchi wa Pemba na mikoa yake miwili kwa kufanya juhudi kubwa za kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kiasi ya kupungua maambukizi yake kwa kiwango kikubwa.

'' Tumefanikiwa kiasi kikubwa Pemba kupambana na ugonjwa wa Covid-19 na kushusha maambukizi yake na kuwafanya wananchi kufanya shughuli zao huku wakiweka tahadhari,'' alisema.

Ametaja siri ya mafanikio hayo ni kufanya ukaguzi wa afya kwa wananchi waliokuwa wakiingia kisiwa cha Pemba zaidi kutoka Tanga na Mombasa, Kenya ambapo ugonjwa huo umeathiri kwa kiasi kikubwa.

Alitoa ahadi ya vifaa hivyo kutumiwa kwa malengo vitanda vitatumiwa kwa wagonjwa watakaolazwa hospitali nne za kisiwa cha Pemba, Chakechake, Wete na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba.

ALIYEKUWA mjumbe wa Taasisi ya Muungano wa Jamii Tanzania (Mujata), ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi