loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ajira viwanda vya mazao ya kilimo zaongezeka

AJIRA katika viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo yakiwemo ya chakula, zimeongezeka kutoka wastani wa watu 3,880,262 hadi kufi kia wastani wa watu 5,204,607 kutokana na wawekezaji 109 waliowekeza katika sekta hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Wizara ya Kilimo wakati ikijibu swali la Mbunge wa Chumbuni, Ussi Salum Pondeza (CCM). Pondeza alisema nchi inatekeleza sera mbalimbali ili kuwa na uchumi wa viwanda. Aliuliza je, serikali ina mikakati gani ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula, matunda na viungo katika kufanikisha sera ya viwanda.

Pia aliuliza kuna wawekezaji wangapi wa mazao ya vyakula ambao wamejitokeza kuwekeza katika sekta ya kilimo tangu kuanza kwa utekelezaji wa mpango wa Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda. Aliuliza, serikali imechukua hatua gani katika kuwaondoa wananchi katika kilimo cha asili na kuwaingiza katika kilimo cha kisasa.

Wizara ya Kilimo ilisema uwekezaji huo, ulifanyika kuanzia 2015/2016 hadi 2019/2020, lakini pia serikali inatekeleza mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo ili kufanikisha sera ya viwanda nchini.

Mikakati hiyo ni pamoja na kuimarisha mfumo wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo kwa kushirikisha sekta ya umma na sekta binafsi. Pia kuendelea kutathmini mahitaji na uwezo wa viwanda na kuviunganisha na wazalishaji wa mazao hayo na kusajili wakulima na wadau wa mazao hayo kwa ajili ya kuratibu uwekezaji na upatikanaji wa huduma na taarifa.

Pia kuendelea kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA na kuimarisha majadiliano na taasisi za fedha ili kuongeza ugharamiaji katika mnyororo wa thamani wa mazao hayo pamoja na kuendelea na majadiliano kati ya serikali na kampuni za bima ili kutekeleza bima ya mazao katika sekta ya kilimo.

Pia serikali inatekeleza mikakati ya kuboresha kilimo nchini ili kuwaondoa wakulima katika kilimo cha asili na kulima kwa mfumo wa kisasa. Mikakati hiyo ni kufanya utafiti wa teknolojia za zana za kilimo katika kulima, kupanda, kuvuna na kusindika.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

1 Comments

  • avatar
    Jack
    29/05/2020

    Hanamkundu atakuwa mtoto wa kichaga kwa ajili ya kufanya operation za sifa wametaka wenyewe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi