loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Halima Mdee ana kesi ya kujibu

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemuona Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee (Chadema) ana kesi ya kujibu baada ya kupitia ushahidi na kujiridhisha.

Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.

Akisoma uamuzi huo jana, Hakimu Mkazi Simba alisema Mdee anakabiliwa na shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli, kosa analodaiwa kulitenda Julai 3, 2017 katika Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Alisema upande wa Jamhuri katika kesi hiyo, walifunga ushahidi Februari 20, 2020 wakiwa na mashahidi watatu, huku upande wa utetezi wakiwasilisha hoja za kuishawishi mahakama imuone mshtakiwa hana kesi ya kujibu.

“Mahakama imepitia kwa makini ushahidi, hoja zilizowasilishwa na msimamo wa kisheria nimejitosheleza kwamba mshtakiwa ana kesi ya kujibu,” alisema Hakimu Mkazi Simba.

Aidha, baada ya uamuzi huo, alimtaka mshitakiwa kueleza atajitetea kwa mfumo upi na iwapo atakuwa na mashahidi, watakuwa wangapi kama ambavyo sheria inataka.

Wakili wa utetezi, Hekima Mwasipo alisema mteja wake atajitetea kwa kiapo na atakuwa na mashahidi watano. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 25 na 26 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa utetezi.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Julai 3, 2017, Mdee akiwa katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mtaa wa Ufipa Wilaya ya Kinondoni, alitamka maneno ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli, kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani. Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Anna Mwikola

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi