loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

NEMC yapongezwa kwa kuanzisha kikosi kazi

OFISI ya Makamu wa Rais imefurahishwa na kulipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kuanzisha kikosi kazi cha dharura, kinachofanya kazi kwa saa 24 na kutatua dharura za kimazingira zinazojitokeza katika jamii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa pamoja kati yake na Bodi ya Wakurugenzi ya NEMC, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Zungu alieleza furaha ya serikali kwa kuundwa kwa kikosi hicho na NEMC chini ya usimamizi wa bodi.

Lakini, alitaka juhudi kubwa ifanywe kusambaza kwa umma elimu na kukaribisha mjadala juu ya kulinda na kuhifadhi mazingira, ili iwe rahisi kusimamia sheria na kanuni za kulinda mazingira.

“Imekuwa siku muhimu kwangu kukutana na Bodi ya Wakurugenzi na kupata fursa ya kupeana mawazo juu ya mambo mbalimbali ya kiutendaji. Tumeangalia madhaifu yaliyopo katika usimamiaji wa sheria, mradi wa vyura wa Kihansi na kero za wadau katika biashara ya chuma chakavu. Naipongeza Bodi kwa jitihadi ilizochukua ikiwemo uanzishwaji wa kikosi kazi cha dharura katika baraza letu (NEMC),” alisema Zungu.

Aliitaka bodi kuendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizopo katika usimamiaji wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 na Kanuni zake.

“Licha ya kazi nzuri ambayo baraza linazifanya, wakati umefika wa kuhakikisha elimu pana inatolewa kwa jamii ili kurahisisha usimamiaji wa sheria na kanuni za mazingira,” alisema Zungu na kuongeza kuwa matokeo ya mjadala huo wa usimamizi wa mazingira, yataanza kuonekana hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Bodi ya baraza hilo, Profesa Esnat Chaggu alisema watayafanyia kazi maelekezo ya waziri kwa lengo la kuleta ustawi wa mazingira nchini.

“Kama bodi tumepokea maelekezo ya waziri na tutaendelea kuchukua hatua zinazostahili ili kuyatunza mazingira yetu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kesho,” alisema Profesa Chaggu.

Alisema kikao cha pamoja kimekuwa cha manufaa kwa taifa, na kitaongeza ufanisi, kwa vile kimejadili mambo muhimu ambayo yakisimamiwa vyema na watendaji wa NEMC yatachochea kasi ya kusimamia Sheria ya Mazingira na Kanuni zake.

Alieleza kuwa licha ya NEMC kuwa na kikosi kazi cha dharura, pia kutakuwepo na gari maalumu ambalo litalifanya baraza, kwa sehemu kubwa, kuwa na picha halisi juu ya hali ya mazingira ilivyo.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi