loader
Dstv Habarileo Mobile
Picha

Akina Samatta kuanza na Sheffield Juni 17

MSIMU wa Ligi Kuu ya England umepangwa kuendelea tena Juni 17, 2020, huku timu ya Mtanzania, Mbwana Samatta itacheza dhidi ya Sheffi eld United wakati Manchester City ikikwaana na Arsenal, imeelezwa.

Aston Villa iko katika nafasi ya 18 baada ya kushuka dimbani mara 28 na imejikusanyia pointi 25 na inahitaji ushindi ili angalau ijiweke katika nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu.

Timu hizo nne kila moja imecheza mechi 28 wakati zingine ilizobaki zina mechi 29, hivyo wameamua kuanza na viporo. Ligi hiyo itaendelea wikiendi ya Juni 19-21, ambapo timu zote zitashuka kwenye viwanja tofauti.

Hadi jana usiku klabu zilikuwa zinaendelea kujadili mambo mbalimbali ya ligi hiyo, iliyobakisha mechi 92 kabla ya kukamilika kwa msimu wa mwaka 2019/2020.

Ligi Kuu ilisimamishwa Machi 13 kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona na hadi inarejea, zitakuwa zimepita siku 100 baada ya Leicester City kuichapa Aston Villa 4-0 Machi 9, huku mechi zote zilizobaki zikipangwa kuchezwa bila ya mashabiki. Jumatano, klabu nyingi zilipiga kura za ndio kuruhusu timu kuendelea na mazoezi ya kugusana, baada ya wiki iliyopita kuanza mazoezi ya kucheza wachezaji bila kugusana.

Hadi sasa, watu 12 wamekutwa na virusi vya corona baada ya watu 2,752 wanaohusika na ligi hiyo kupimwa. Wachezaji wa Ligi Kuu wataendelea kupimwa mara mbili kwa wiki, huku idadi ikiongezeka kutoka 50 hadi 60 kwa klabu katika raundi ya nne ya vipimo.

Liverpool inaoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa pointi 25 kileleni wakati Bournemouth, Aston Villa na Norwich City ziko katika hatari ya kushuka daraja zikiwa na pointi 27, 25 na 21.

LIONEL Messi, alifunga bao lake la 700 katika historia yake ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

2 Comments

 • avatar
  Jack
  29/05/2020

  Hana ###### atakuwa mtoto wa kichaga kwa ajili ya kufanya operation za sifa wametaka wenyewe..

 • avatar
  Jack
  29/05/2020

  Hanamkundu atakuwa mtoto wa kichaga kwa ajili ya kusfanya operation za sifa wametaka wenyewe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi