loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pinda aipa SUA ekari 200 za ardhi kwa kilimo

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amekikabidhi Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kampasi ya Mizengo Pinda Katavi, ekari 200 za ardhi katika kijiji cha Milolo zitakazotumika kwa wanafunzi wa chuo hicho kufanya mazoezi kwa vitendo.

Pia Pinda ametoa majengo katika eneo la Mpimbwe lenye ekari 64 ambayo yataanza kutumika kama Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Kampasi ya Mizengo Pinda.

Mratibu mwanzilishi wa kampasi hiyo, Dk Beno Mlembuka alisema wataanza kupokea wanafunzi kwa mara ya kwanza Novemba mwaka huu ambao ni wanafunzi 300 wa stashahada ya Ufugaji nyuki pamoja na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Alisema uongozi na baraza la chuo umeridhia kupokea wanafunzi baada ya kukamilika miundombinu ya chuo ambacho kitakuwa chuo cha kwanza katika mkoa wa Katavi. Aidha Dk Beno ameishukuru serikali kwa kukubali maombi ya kutoa fedha zaidi ya Sh milioni 350 kwa ajili ya ukarabati wa chuo hicho ambacho mara kitakapoanza itakuwa ni fursa kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na mikoa mingine ya ukanda wa magharibi.

Pia alisema chuo hicho ni fursa kwa wakulima wa mkoa huo kwani wanafunzi watahitaji huduma mbalimbali, hivyo wakulima nao kuwa na uhakika wa soko la kuuza mazao yao.

Alisema, uwepo wa chuo hicho Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika kijiji cha Kibaoni utabadili Halmashauri ya Mpimbwe na sura ya mkoa mzima wa Katavi. Mkuu wa mkoa huo, Juma Homera alisema chuo hicho kinaufanya Mkoa wa Katavi kufikisha vyuo vinne kikiwemo Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Chuo cha Afya, Veta.

Homera alisema, uwepo wa chuo hicho utakuwa ni fursa nyingine kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi kunufaika kiuchumi kwani vijana watapata nafasi ya kusoma hivyo kuwa na uhakika wa kupata wasomi wengi ambao watakwenda kufanya kazi katika mkoa huo.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Mpimbwe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi