loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watumishi 6 manispaa mbaroni kutowasilisha milioni 25.5/-

JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watumishi sita wa Halmashauri ya Manispaa Tabora kwa tuhuma za kutowasilisha benki mapato ya Sh milioni 25.5.

Agizo la kukamatwa watumishi hao limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini, Komanya Kitwala baada ya kumalizika kikao cha dharura cha watumishi alichokiitisha na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, Bosco Ndunguru, mhasibu Amran Mteta na baadhi ya watendaji hao.Watumishi wanne walikamatwa papo hapo.

Kitwala aliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka watumishi wengine wawili ambao hawakufika wakiwemo vibarua watano wanaotuhumiwa kukusanya Sh milioni 1.2 na kutoroka nazo.

Alifafanua kuwa watumishi hao wanakwamisha juhudi za maendeleo katika manispaa hiyo ndio maana aligiza Ofisi ya Mkurugenzi kumletea orodha ya watumishi wote waliokusanya mapato hayo na kutoyawasilisha benki ili sheria ichukue mkondo wake.

Alisema kuwa mtumishi yeyote aliyepewa dhamana na serikali anapaswa kutekeleza wajibu wake ipasavyo na sio kufanya ujanja ujanja katika kukusanya mapato ya serikali. Awali Ndunguru alisema kukabidhi majina hayo kulifuatia maazimio ya kikao cha Kamati ya Fedha Mei 22, 2020 kujadili taarifa ya mapato na matumizi ya halmashauri.

Alisema baada ya kupitia nyaraka za mapato yaliyoingizwa benki, kamati ilijiridhisha pasipo shaka kuwa watumishi hao saba na vibarua watano hawakupeleka benki fedha zote walizokusanya, hivyo wakaazimia kuwasilisha majina yao kwa Mkuu wa Wilaya.

Mhasibu wa manispaa, Amrani Mteta alitaja watumishi wanaotuhumiwa kutowasilisha mapato ya halmashauri benki ni Ofisa Kilimo Richard Mkama (Sh mil 2.3), mlinzi Salumu Daud (Sh milioni 12.28) na Mtendaji wa kata, Abdallah Mgemwa (Sh mil 2.6).

Wengine ni Mtendaji wa Mtaa, Savela Fimbo (251,200), Mtendaji wa Mtaa- Hamis Abdul (310,000), Ofisa Mifugo, Cornelius Masawe (Sh milioni 7.5) na Mtendaji wa kata Cesilia Ernest (21,000) ambaye amelipa kwa kuchelewa hivyo kutakiwa kupewa onyo.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

1 Comments

  • avatar
    james mcshija
    29/05/2020

    inatia hofu sana! mpaka kiasi hicho ninachukuliwa kweli? "no check up". nani wakupewa rawama? mpaka mlinzi anakuzanya fedha?

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi