loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Trump atishia kufunga mitandao ya kijamii

DONALD Trump jana alitarajia kutia saini agizo linalolenga kuifungia mitandao ya kijamii na kampuni za mitandao hiyo, kwa tuhuma za kuwa inajaribu kuzuia uhuru wa kujieleza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Marekani, Rais Trump amefikia uamuzi huo baada ya kuibuka kwa mzozo mapema wiki hii, ambapo mtandao wa kijamii wa Twitter ulihakiki baadhi ya ujumbe wa Rais huyo. Rais Trump ni miongoni mwa viongozi wanaopenda kutumia mtandao wa Twitter kufikisha ujumbe wake kwa watu.

Hata hivyo, kiongozi huyo alikasirika kwa mara ya kwanza baada ya mtandao huo kubadilisha baadhi ya maneno aliyoandika kwenye ukurasa wake na hivyo kupotosha maana. Rais Trump alisema kufanya hivyo ni kuingilia kati uhuru wa kujieleza wa mtu, jambo ambalo ni hatari.

Twitter ilichukua hatua hiyo ambayo haraka ilichochea mvutano kati yake na Rais Trump, baada ya Rais huyo wa Marekani kuandika Tweet mbili, akidai kwamba mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta una udanganyifu mwingi. Ilichofanya Twitter ni kuweka kiungo kingine chini ya ujumbe wa Trump kinachosema: “Pata taarifa za ukweli juu ya kura ya njia ya posta,” na baadae kiungo hicho kinampeleka mtumiaji kwenye makala ya habari inayompa taarifa za ukweli kuhusu suala hilo na orodha ya maelezo yanayopinga madai ya Trump.

Rais Trump mwenye wafuasi wapatao milioni 80 katika ukurasa wake wa Twitter, anasema anautumia mtandao huo wa kijamii kupinga kile anachodai kuwa ni taarifa za upendeleo zinazotolewa na vyombo vya habari.

Kiongozi huyo amekuwa akidai kwamba, mtindo wa kupiga kura kwa njia ya posta, una viwango vya juu vya udanganyifu katika wakati ambapo majimbo mengi yanazingatia kuitumia ili kulinda afya ya raia dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa covid-19, wakati taifa hilo likiwa linaelekea katika uchaguzi wa Rais wa Novemba, mwaka huu.

JESHI la Polisi kupitia Kikosi cha Farasi, limeanzisha huduma ya ...

foto
Mwandishi: WASHINGTON, Marekani

1 Comments

  • avatar
    hussein
    29/05/2020

    benafsi nadhani bwana trump yupo sahihi juu ya upigaji kura wakutumia njia ya posta utakiuka sheria na haki ya mpiga kura njia hii lazima ichunguzwe kiufasaa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi