loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ukerewe yashusha ushuru wa samaki kuvutia uwekezaji

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, imeshusha viwango vya ushuru wa samaki, kwa lengo la kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo na kuongeza mapato.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Diwani wa Kata ya Bukanda, Willbrod Mbando kutoa hoja katika baraza la madiwani jana, akitaka viwango vya ushuru wa samaki na dagaa, viangaliwe upya ili kunusuru mapato ya halmashauri hiyo.

“Mwenyekiti tangu viwango vya ushuru vipandishwe Septemba mwaka jana baadhi ya wavuvi na wanunuzi wa samaki wamehama huku baadhi yao wakitorosha samaki na kuuza wilaya jirani kwa kukwepa viwango hivyo vya ushuru, hali ambayo inaikosesha mapato halmashauri,”alisema Mbando.

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Cornel Magembe akizungumza katika kikao cha wadau wa uvuvi hivi karibuni, alitaka halmashauri hiyo kupunguza viwango vya ushuru ili kunusuru mapato yake, ambapo Julai hadi Desemba 2019 ilikusanya asilimia 18 ya mapato ya vyanzo vya ndani.

“Nalipongeza baraza hili kwa kuliona hili kwa sababu halmashauri ilikuwa inakosa mapato kwa kukimbiwa na wadau wa sekta hiyo hivyo kudumaza huduma kwa wananchi,”alisema.

Akifafanua suala hilo, Mwanasheria wa halmashauri hiyo, alisema viwango vya ushuru vinatozwa kwa mujibu wa sheria, lakini baraza la madiwani linaweza kupitisha azimio la kushusha viwango hivyo kwa muda wakati mchakato wa kisheria wa kubadili sheria ukifanyika.

Alisema madiwani ndio wenye mamlaka ya kupitisha sheria na miongozo ya kuendesha halmashauri, hivyo kama wamebaini tozo hizo zinaathiri mapato wanaweza kusimamisha kwa muda sheria ya tozo hizo na kupendekeza viwango vingine.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, George Nyamaha akitangaza viwango vipya vilivyoridhiwa na baraza la madiwani, alisema wamekubaliana viwango vipya vya ushuru, vitozwe katika kipindi cha mwaka mmoja wa fedha kuanzia Julai 2020 hadi Juni 2021.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Jovither Kaijage, Ukerewe

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi