loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ZAFICO yaanza uvuvi bahari kuu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesema Shirika la Uvuvi la Zanzibar (ZAFICO) kwa kutumia meli yake aina ya Sehewa II iliyonunuliwa kutoka nchini Srilanka imeanza shughuli za uvuvi katika eneo la ukanda wa bahari kuu lenye utajiri mkubwa wa samaki.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mmanga Mjengo Mjawiri akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo mwaka wa fedha 2020/2021.

Alisema uvuvi eneo la bahari kuu utaliwezesha Shirika la Uvuvi kuuza samaki ndani ya nchi katika soko la utalii na kusafirisha nje ya nchi. Alisema kuanzishwa kwa shirika hilo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kuona sekta ya uvuvi inaleta tija kwa taifa pamoja na kuwawezesha wananchi kuunda vikundi vyao vya uvuvi.

Alisema kuwepo kwa shirika hilo kwa kiasi kikubwa kutaifanya sekta ya uvuvi kuongeza mchango wake kwa uchumi kwa taifa. “Nampongeza Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kufufua Shirika la Uvuvi (ZAFICO) lifanye kazi za uvuvi mwambao wa bahari kuu kumaliza uhaba wa samaki,’’alisema.

Aidha alisema ZAFICO inatarajiwa kununua boti nyingine tano za uvuvi kwa vikundi vya vijana maeneo ya ukanda wa bahari kuu na doria.

Alisema Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha uvuvi haramu unaotumia mitego iliyozuiwa unadhibitiwa. Alisema wanakabiliana na uvuvi haramu kwa kufanya doria 172 maeneo yaliyotengwa ya hifadhi ya uvuvi mwambao Unguja na Pemba.

Alizitaja doria hizo ikiwemo ya ukanda wa hifadhi ya PECCA Pemba ambapo doria 30 zilifanyika huku ukanda wa hifadhi ya MIMCA iliopo Unguja jumla ya doria 41 zilifanyika.

Katika doria hizo, mitego ya samaki haramu 68 ilikamatwa na kuharibiwa ikiwemo nyavu zenye macho madogo zinazonasa samaki mbali mbali ambao hawafai kwa matumizi ya binadamu. Alizipongeza kamati za uvuvi za halmashauri ya vijijini zilizofanya kazi kubwa kupambana na uvuvi haramu ikiwemo kusaidia kazi za doria.

“Tumedhibiti uvuvi haramu uliokuwa tishio kwa kuharibu rasilimali za baharini ikiwemo samaki na matumbawe kwa kutumia kamati za halmashauri za vijiji hifadhi ya uvuvi,”alisema.

Aliomba Baraza la Wawakilishi kuidhinisha Sh bilioni 129.89, ambapo Sh bilioni 23.32 kazi za kawaida na Sh bilioni 6.63 kwa ajili ya ruzuku, kazi za utafiti wa uvuvi na mazao ya baharini.

Rais John Magufuli amemteua Dk Philemon Sengati kuwa Mkuu wa ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi