loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TBL, TARI wazalisha mbegu bora za mtama

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafi ti wa Kilimo Tanzania (TARI), zimefanya utafi ti na kuibuka na mbegu bora za mtama kwa ajili ya matumizi ya uzalishaji wa bia.

Utafiti huo umefanyika kupitia mradi shirikishi wenye lengo la kuwawezesha wakulima wa mtama nchini kuongeza uzalishaji. Kupitia mradi huo, mbegu zinazalishwa kwa kutumia utaalamu wa kisasa, ambao unawezesha kuongeza mavuno kwa asilimia 43, tofauti na uzalishaji unaotumika kwa kutumia njia nyinginezo.

Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman, alisema jana kuwa utafiti wa uzalishaji mbegu bora, ulianza mwezi Desemba mwaka jana katika maeneo ya Hombolo, Kibaigwa na Kongwa mkoani Dodoma. Alisema utafiti huo utawezesha kupata mbegu bora za mtama, kwa ajili ya kusambaza maeneo mengineyo nchini.

“Kupitia mradi huu, wakulima wa mtama watapatiwa ushauri wa kilimo bora kutoka kwa wataalamu wetu na lengo letu kubwa ni kuwawezesha wakulima wa mtama kupata mavuno mengi zaidi, kutumia maji kidogo na kuwawezesha kuwa na bima ya kuwakinga na changamoto za kilimo” alisema.

Redman alisema mbali na kuinua maisha ya wakulima, pia kupitia mradi huo kampuni itapata malighafi ya uzalishaji wa bia zake za gharama nafuu za Eagle Lager na Bingwa.

Alisema tayari kampuni imejipanga kununua asilimia 74 ya malighafi nchini na itaendelea kununua malighafi zake zote kutoka hapa nchini katika kipindi cha miaka ijayo.

Kwa upande wake, Meneja wa TARI Hombolo, Dk. Lameck Makoye, alisema kuwa mradu huo utawezesha wakulima kupata mbegu bora za mazao, ambazo zinawawezesha kupata mavuno zaidi ya mtama na kuboresha maisha yao.

JESHI la Polisi kupitia Kikosi cha Farasi, limeanzisha huduma ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi