loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Corona yaua waandishi 20 Amerika

CHAMA cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo cha Amerika (AIPS), ndio kimeathirika zaidi na ugonjwa wa Covid-19 si tu kwa sababu za kiuchumi, lakini baada ya kupoteza waandishi wake kutokana na ugonjwa huo.

Ugonjwa huo umegharimu maisha ya waandishi wake 20 wa michezo, ambao saba kutoka nchini ya Ecuador na 13 Peru.

Waandishi hao walipewa heshima Jumamosi iliyopita wakati wa mkutano wa kwanza wa Kamati ya Utendaji ya AIPS Amerika.

Kabla ya kuanza kwa mkutano huo ulioendeshwa kwa njia ya video, viongozi na wajumbe wake walisimama kimya kwa dakika moja wakitoa heshima kwa wote walikufa tangu Machi hadi sasa, kwa mujibu wa kiongozi mmoja.

BOLIVIA

Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo cha Bolivia kimethibitisha kifo cha kwanza cha mwandishi wake kutokana na COVID-19, Jacinto Quispe, ambaye ni produza na mpiga picha, aliyefanya kazi nyingi za uandishi wa habari nchi humo, ambaye hivi karibuni alikuwa na kazi ya michezo.

Mwandishi huyo alifariki dunia huko Santa Cruz – jiji ambalo limeathirika zaidi na janga hilo nchini humo.

PERU

Huko Peru, mwandishi Raúl Dreyfus alifariki akiwa na umri wa miaka 96, kutokana na matatizo ya moyo. Raúl alikuwa mmoja wa waandishi wenye uwezo na mzoefu katika uandishi wa michezo nchini humo.

MITAA ya mji wa Ruangwa imepambwa kwa bendera za rangi ...

foto
Mwandishi: BOGOTA, Colombia

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi