loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CAF yagawa mamilioni kwa wanachama

SHIRIKISHO la Soka Afrika (Caf) litatoa kiasi cha Dola za Marekani milioni 10.8 (sawa na Sh trilioni 23) kwa ajili ya wanachama wake kupunguza makali ya ugonjwa wa COVID-19, imeelezwa.

Kikao cha dharura cha Caf kilichofanyika juzi kwa njia ya video kiliidhinisha fedha hizo na kusema zitolewe kwa haraka katika mashirikisho ya soka ya nchi za Afrika (MA) ili kusaidia katika maeneo yao yaliyoathirika zaidi.

Kila mwanachama wa Caf, likiwemo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anatarajia kupata zaidi ya Sh milioni 185.1 kama msaada wa fedha kusaidia vyama vya soka vya mikoa.

“Jumla ya kiasi cha Dola za Marekani milioni 10.8 zitapelekwa kwa Mashiriksho ya Soka 54 barani Afrika ikiwa ni sehemu ya kupunguza makali katika jamii ya soka katika kipindi hiki kigumu, “ilisema taarifa hiyo.

“Kutokana na kusambaa kwa haraka kwa ugonjwa wa COVID-19, Mashirikisho ya Soka ya Afrika yalisimamisha mahindano yote, na kusababisha tatizo kubwa la fedha. Caf imeamua kupunguza mzigo huo, “alisema Rais wa Caf Ahmad Ahmad.

Pia Caf imekubali kusaidia tena MA ili viweze kuendelea na mashindano ya nyumbani.

Wiki mbili zilizopita, CAF ilitangaza mgao wa kiasi cha Dola za Marekani milioni 3.5 (sawa na Sh bilioni 8.1) kwa klabu zinazoshiriki katika michuano ya Afrika msimu wa mwaka 2019/20.

Mashindano hayo mawili ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika na yale ya Kombe la Shirikisho Afrika, yalisimamishwa baada ya mechi za hatua ya robo fainali kutokana na mlipuko wa COVID-19.

Wakati huohuo, Caf wanafuatilia kwa ukaribu na kufanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Fifa kuhusu athari za corona barani Afrika, na itatangaza maendeleo kuhusu mashindano ya Afrika katika muda muafaka ili kujua yatarejea lini.

MITAA ya mji wa Ruangwa imepambwa kwa bendera za rangi ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi