loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Corona yafuta Boston Marathon 2020

BOSTON Marathon sasa imefutwa kabisa ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 124 ya historia ya mbio hizo kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Awali, mbio hizo zilipangwa kufanyika Aprili 20 kabla ya kuahirish- wa hadi Septemba 14 mwaka huu, lakini sasa waandaaji wameamua kuyafuta kabisa.

Hata hivyo, Meya wa Boston Marty Walsh alisema mbio hizo hazitafanyika tena mwaka huu kwa sababu ya hatari ya kiafya.

“Hakuna njia, hatutaweza kuandaa tena mbio hizo za kila mwaka, ambazo zimekuwa zikishirikisha watu wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani”, alisema Walsh juzi.

Hizo ndio mbioni za muda mrefu zinazofanyika kila mwaka duniani, ambapo zimekuwa zikifanyika tangu zilipoanza mwaka 1897 na hazikuwahi kutofanyika hata mara moja.

Mkenya Lawrence Cherono na Worknesh Degefa wa Ethiopia ndio washindi kwa upande wa wanaume na wanawake wa mbio za mwaka 2019.

Kwa mujibu wa waandaaji wa Boston Marathon, washindi wa mwaka jana wa mbio hizo, Mkenya Cherono na Worknesh wa Ethiopia kila mmoja aliondoka na Dola za Marekani 150,000 (ambazo ni sawa na Sh milioni 432.3).

Washindi wa pili kila mmoja alipata Dola za Marekani 75,000 wakati watatu waliondoka na kitita cha Dola 40,000.

Katika mbio hizo za mwaka jana zilizofanyika Aprili 15, Cherono alimaliza wa kwanza kwa kutumia saa 2:07:57 wakati mwanadada Degefa alishinda kwa wanawake kwa kutumia saa 2:23:31.

MITAA ya mji wa Ruangwa imepambwa kwa bendera za rangi ...

foto
Mwandishi: BOSTON, Marekani

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi