loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Madee- Tumeiba sana Manzese

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Hamad Ally Seneda, ‘Madee’ amesema wameiba sana na walikuwa wakijiita Muslim by Nature.

Madee aliyasema hayo pamoja na mambo mengine yahusuyo muziki na maisha yake katika kipindi cha SalamaNa kinachorushwa na EATV juzi usiku.

“Tumeiba sana, ila ningeendelea ningekuwa mwizi sana, tulikuwa tunaiba Manzese tena tulikuwa tunajiita Muslim by Nature, kipindi hicho wahuni wote walikuwa wanapatikana Manzese kuchukua mitumba,” alisema Madee.

Madee ambaye anajulikana kama Rais wa Manzese chini ya Kkundi la Tip Top Connection alisema baba yake Mzee Seneda alikuwa mwanamuziki wa Tabora Band lakini hakupata mafanikio na wakati yeye anaanza ilibidi akimbienyumbani maana baba yake alikuwa hataki awe msanii.

“Baba yangu alikuwa mwanamuziki anaitwa Seneda, lakini hakupata mafanikio, wakati naanza muziki nilikimbia nyumbani maana alikuwa hataki niwe msanii,” alisema.

Pia alisema kuwa na watoto nje ya ndoa hakumsumbui bali kunamkuza ili akiingia kwenye ndoa ajifunze jinsi ya kuishi na vitu vinavyotokea duniani.

“Hainisumbui kuwa na watoto nje ya ndoa ila inanikomaza zaidi hata nikiingia kwenye ndoa nijifunze jinsi ya kuishi na vitu vinavyotokea duniani na namna ya kumlea mtoto aliyeko nje ya ndoa ni kumuonesha upendo maana akiwa na mama yake hujui wanaongea nini, hivyo muoneshe wewe ndio baba yake,”

Aidha, ametoa ahadi ya zawadi ya Sh 300,000 kwa mtu atakayemletea video yake ya wimbo wa Mola auweke kwenye You- Tube na kusema wimbo huo ulimpatia pesa akanunua kiwanja.

“Nimetoa ahadi ya kutoa 300,000 kwa mtu atakay- eniletea video yangu ya kazi yake Mola maana nataka niiweke kwenye YouTube Channel yangu, nahisi huo wimbo unahitajika, wimbo huo ulinipa pesa nikanunua kiwanja nikakiacha kwa miaka 10 au 15, nilivyopata pesa wimbo wa Pombe Yangu, nikajenga, nina bonge la mjengo” aliongeza.

Madee alisema siri ya wimbo wa kazi yake mola kufanya vizuri mpaka sasa ni kutokana na kutuliza kichwa wakati anaandika mashairi yake tofauti na vijana wa sasa, ambao wanaingia studio wakiwa hawajui wanataka kuimba nini.

MITAA ya mji wa Ruangwa imepambwa kwa bendera za rangi ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi