loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanawake msibweteke corona bado ipo

HABARI muhimu na za kutia moyo ni kupungua kwa maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya mapafu Covid-19 nchini jambo lililosababisha baadhi ya shughuli kurejea ambazo zilisimama kwa miezi kadhaa.

Hatua ya kurejea kwa shughuli pamoja na kubaki wagonjwa wanne katika hospitali za jiji la Dar es Salaam, ni mwanga kwa kumalizika kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Licha ya kupungua kwa wagonjwa bado wataalamu wa afya wanasisitiza kuwepo kwa ugonjwa huo nchini hivyo ni vema watu wakaendelea kuchukua tahadhari na hatua madhubuti za kujikinga ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka misongamano pamoja na kuvaa barakoa pale inapolazimu kutoka nje.

Kutokana na ushauri wa wataalamu wa kutaka watu waendelee kujikinga lakini jambo la ajabu ni kuwa wapo baadhi ya wanawake licha ya kuacha kunawa mikono mara kwa mara wamekuwa na safari zisizo na msingi tena kwenye maeneo ya misongamano bila kuvaa barakoa.

Mbaya zaidi wanaporejea nyumbani hawakumbuki kunawa mikono, kupaka vitakasa mikono na huingia ndani jambo ambalo ni hatari wanaweza kupeleka maaambukizi mapya majumbani.

Ni vema wanawake wakatambua kuwa ugonjwa huo bado upo mpaka pale wataalamu watakapotangaza kuisha kabisa ndipo waache kujikinga lakini hadi sasa bado tunasisitiziwa umuhimu wa kujikinga kwa kufuata hatua zote za msingi ambazo wataalamu wa afya wamekuwa wakifundisha ama kuelekeza.

Wanawake mna wajibu wa kulinda familia, ni vema mkaendelea kusimamia suala la kujikinga ndani ya familia zenu kwa kuchukua hatua zote ikiwemo watoto kutoruhusiwa kutoka nje na kwenda kwenye mikusanyiko ya watoto mitaani..

Siku hizi si ajabu kukuta na wanawake wakiwa katika makundi wakati awali hata katika vikundi vya maendeleo walitumia mitandao ili kufanya shughuli zao za maendeleo huku wakichukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu.

Pia kumekua na watoto mitaani, tena wamerejea kwa kasi wakikusanyana na kucheza kwa makundi kwa madai ya ugonjwa wa Covid-19 umekwisha jamboo ambalo si kweli.

Lakini pia wananchi wakiwemo wanawake wakitembea mitaani bila kuvaa barakoa wakiwa katika mikusanyiko au vyombo vya usafiri vya umma.

Ni vema kuendelea kuchukua hatua kuepuka maambukizi mapaya hasa wakati huu kuna matumaini ya kupungua kwa ugonjwa huo kwani bila kuchukua tahadhari ya kujilinda yanaweza kusababisha mlipuko mwingine wa maambuziki ya corona.

Kipindi hiki ambacho wanafunzi wa vyuo vikuu na kidato cha sita wamerejea katika masomo, huku wanafunzi wa shule za awali, msingi na sekondari wakitarajia kurejea shuleni ni vema wanawake wakaendelea kuzipa familia zao vyakula vyenye kuendelea kuongeza kinga.

UZURI wa ngozi huanzia ndani. Hivyo unavyoitunza ngozi yako kwa ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi