loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watu watatu katika shambulizi dhidi ya Mbowe

JESHI la Polisi mkoani Dodoma, limethibitisha kutokea tukio la shambulizi leo alfajili, dhidi ya Kiongozi wa Kambi Kuu ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto, Mbowe alishambuliwa alipokuwa akipandisha ngazi kuelekea nyumbani kwake muda mfupi baada ya kushuka kwenye gari. Inaelezwa kuwa watu waliovalia jaketi, walimshambulia kwa mateke, usiku wa saa sita na amejeruhiwa mguu wake wa kulia.

“Alfajili ya leo tulipokea taarifa kutoka kwa mbunge viti maalumu na dereva wa mheshimiwa Mbowe, kuwa mbunge alikutana na watu watatu waliokuwa wamevaa jaketi na walimshabulia kwa mateke na amejeruhiwa mguu wake wa kulia” alisema.

Aidha kamanda Muroto ameongeza kuwa tukio hilo linachunguzwa na polisi na kuwaonya wale wote wanaotaka kutumia tukio hilo kama mtaji wa kisiasa.

“Onyo ni watu kutumia tukio hili kama mtaji wa kisiasa, lakini pia tunaona kwenye mitandao ya kijamii wanahamasishana, kukutana kwenye ofisi za chama cha CHADEMA, yeyote atakaye vunja sheria kwa mikusanyiko isiyo halali, kwa uchochezi kwa njia ya maandishi ambao hauzingatii sheria, atashughulikiwa” aliezeka Muroto.

MBUNGE wa Mbeya mjini Dk Tulia ...

foto
Mwandishi: Tagato James

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi