loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mo Simba Arena wafungiwa

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeufungiwa Uwanja wa Mo Simba Arena kutumika kwa michezo ya kirafi ki kwa sababu za kiusalama na kutengua katazo la mechi za kirafi ki baada kuzungumza na timu za Ligi Kuu za Dar es Salaam.

Juzi TFF ilitoa tangazo la kuzuia mechi za kirafiki na kuziita timu za Simba, Yanga, Azam, KMC na Transit Camp, ambazo jana ziliitika wito huo na kuzungumza nazo na kukubaliana kutekeleza kanuni za afya kikamilifu.

Hatua ya kufungia uwanja wa Simba ni kutokana na sababu za kiusalama hasa kipindi hiki cha uwapo wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona na pia uwanja huo ulijengwa kwa ajili ya mazoezi lakini juzi ulitumika kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya KMC na Transit Camp na mashabiki kuhudhuria kwa wingi bila kuchukua tahadhari za kujikinga na virusi vya corona.

Awali, serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Wazee na Watoto, zilitoa mwongozo wa namna watu watakavyoingia viwanjani kwa kuzingatia umbali ili kuepukana msongamano.

“Tulikuwa na kikao na klabu zilizocheza mechi za kirafiki kwa sababu katika mechi zao zilizopita hawakuzingatia mwongozo wa serikali, tulijadiliana wakasikitika kwa makosa waliyofanya na kuomba radhi,” alisema Rais wa TFF, Wallace Karia.

Karia alisema wamezungumza na Simba na wamekiri kuwa kitendo cha kutumia uwanja wao ni uharibufu mkubwa wa miundombinu na kukubaliana hawatarudia tena kucheza mechi katika uwanja huo.

Pia alisema wamekubaliana ligi itakapoanza kila timu iunde kikundi maalum cha mashabiki na kuita ‘Social distance agent,’ ambacho kitakuwa na jezi maalum na kitatumika kuhamasisha wenzao umuhimu wa kutokaribiana.

Karia aliwahimiza mashabiki watakaokuwa wanaingia viwanjani kufuata maelekezo ya serikali ya kukaa mbali kati ya mt una mtu, kunawa mikono na sabuni na maji tiririka na kuwasihi maofisa habari wa klabu kuendelea kutoa elimu kwa mashabiki.

Aidha, Karia alisema michezo ya kirafiki imeruhusiwa kuendelea baada ya juzi kutangaza kuifungia, lakini sasa itaruhusiwa kwa kibali maalumu ili kuhakikisha mwongozo wa afya unazingatiwa.

STAA wa Bongo Fleva, Rajab Kahali au Harmonize, ametoa ushauri ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi