loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM aahidi makubwa sanaa, michezo

KUTOKANA na sekta za sanaa, michezo na burudani kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi, serikali imejipanga kuweka mkazo katika miaka mitano ijayo.

Hayo yalisemwa na Rais John Magufuli, wakati akihutubia Bunge la 11, jijini Dodoma jana.

Alisema sekta hiyo licha ya kutosemwa sana, taarifa za hali ya uchumi ya mwaka 2018, imeonesha shughuli za sanaa na burudani ziliongoza kwa asilimia 13.7.

Pia alisema sekta hiyo kwa mwaka 2019 ilishika nafasi ya tatu kwa ukuaji kwa asilimia 11.2.

“Hongereni sana wasanii wetu mbalimbali hususani wa Bongo fleva, filamu, michezo mbalimbali, kazi zenu siyo tu zinaburudisha na kuchangia ukuaji wa uchumi, lakini pia zinaitangaza nchiyetu kimataifa,” alisema.

Pia, aliipongeza timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’ kwa kufuzu Fainali za Afrika mwaka jana baada ya miaka 39 na wanamichezo wengine waliopeperusha vyema bendera ya taifa katika miaka mitano hususan ndondi na riadha.

“Kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na wasanii na wanamichezo nchini, serikali imejipanga katika miaka mitano ijayo kuweka mkazo mkubwa zaidi kwenye sekta hiyo ambayo imeajiri vijana wetu wengi,” alisema.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi