loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba hesabu kwa Mwadui

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Sven Vandenbroeck, amesema kikosi chake kina morali ya kupambana na kupata ushindi kwenye michezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC, utakaofanyika Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sven ametoa kauli hiyo ya kujipa matumaini, akiwa na kumbukumbu ya kikosi chake kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mechi iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja huo wa nyumbani.

Akizungumza Dar es Salaam, Sven alisema licha ya kupata sare kwenye mechi iliyopita, wachezaji wake wana morali na ari ya kupambana kwenye mechi zilizobaki na kupata ushindi ili kutetea ubingwa.

“Bado kuna matumaini ya kufanya vizuri, wachezaji wanaonesha wana jambo ambalo wamepania kulifanya na naona kujituma kwao kwenye mazoezi kwa kufuata maelekezo ninayowapa, nadhani itawafanya waendelee kutafuta ushindi,” alisema.

Aidha, Sven alisema ushindi walioupata wa mabao 4-0 dhidi Transit Camp kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Uhuru, ulikuwa maalumu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mwadui FC, hivyo wana uhakika wa kushinda mchezo huo wa ligi.

Alisema ushindi huo ulikuwa ni muhimu kufuta rekodi ya sare kwenye mchezo uliopita ambao matarajio yao yalikuwa ni kufanya vizuri ili kuanza upya kwenye michezo iliyosalia kwenye ligi hiyo.

Simba inashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 72, baada ya kucheza michezo 29 na kufunga mabao 64 katika michezo 29 waliyocheza. Sasa wanajiandaa kucheza na Mwadui ambayo iliifunga Simba katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Kambarage, mkoani Shinyanga, hivyo wana kazi ya kulipa kisasi

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi