loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bosi mpya Yanga aahidi makubwa

KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Simon Patrick, amesema nafasi aliyopewa anaimudu, hivyo watarajie makubwa kwenye kipindi chake cha utendaji.

Patrick ambaye ni mwanasheria, anakaimu nafasi hiyo baada ya kufutwa kazi kwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, David Ruhago, kutokana na kudaiwa kushindwa kuendana na kasi ya kuisimamia timu ikiwamo kuingia kwenye mfumo wa kisasa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Patrick aliushukuru uongozi wa Yanga kwa kumwamini na kusema viatu alivyopewa anavimudu, hivyo wanachama na wapenzi wa timu hiyo watarajie makubwa kwenye kipindi chake.

“Najua naweza na nitamudu majukumu yangu kwa ufanisi na kasi ambayo Wanayanga wanatamani kuiona na najiamini na nitafanya makubwa kwa maendeleo ya timu katika kipindi changu,” alisema.

Patrick anakabiliwa na majukumu mazito ikiwamo kuhakikisha Yanga inaingia kwenye mfumo wa kisasa wa uendeshaji na kuhakikisha kikosi hicho msimu ujao kinafanya vyema na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa kipindi cha misimu miwili mfululizo.

Nafasi ya Katibu Mkuu Yanga imeendelea kuwa na sintofahamu, kwani tangu alipojiuzulu Charles Mkwasa ambaye alidumu kipindi kirefu, waliofuata wamekuwa hawadumu kwa muda mrefu.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi