loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Azam FC waipania Yanga

TIMU ya Azam FC imepania kuibuka na ushindi kwenye mchezo unaokuja wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga utakaofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi cha Azam ambacho kilitoka kuibuka na ushindi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mbao FC kwa mabao 2-0, kimeanza maandalizi na kina ari kubwa ya kuibuka na ushindi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, kocha wa kikosi hicho, Mromani Arastica Cioaba, alisema kikosi chake kimejipanga kuvuna ushindi kwenye mchezo huo, licha ya ugumu anaotarajia kukutana nao dhidi ya timu hiyo yenye wachezaji wengi nyota.

“Timu yangu imejipanga kupata ushindi dhidi ya Yanga, tumeanza kwa kupata ushindi kwenye mechi iliyopita (Mbao) na tunahitaji matokeo mazuri katika mechi inayokuja ili kuendelea kujikita katika nafasi ya pili,” alisema.

Cioaba alisema mchezo huo utakuwa mgumu, lakini kwa jinsi walivyojipanga, wanatarajia kuondoka na pointi zote tatu na kufikisha 60 na kuendelea kujikita katika nafasi hiyo ya pili.

“Utakuwa mchezo mgumu kwani wote tunapigania nafasi ya juu, ni jukumu letu kama timu kutimiza majukumu yetu ili kuhakikisha tunaibuka na ushindi dhidi ya Yanga,” alisema Cioaba.

Hadi sasa kwenye msimamo wa ligi, Azam wanashika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi 57 walizozikusanya kwenye michezo 29, huku wapinzani wao Yanga wakishika nafasi ya tatu kwa jumla ya pointi 54 baada ya kucheza mechi 27.

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi