loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wamikili Azam Complex wapongezwa

MSIMAMIZI wa kituo cha Dar es Salaam, Lameck Nyambaya ameupongeza uongozi wa Uwanja wa Azam Complex kwa namna walivyoandaa uwanja na kwa kufuata mwongozo wa afya uliotolewa na serikali katika michezo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nyambaya alisema anashukuru kuona wamiliki wa viwanja binafsi kama Azam Complex kufanya kile kilichofanywa Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Simba na Ruvu Shooting.

“Nichukue nafasi hii kupongeza uongozi wa Uwanja wa Azam Complex katika mchezo, ambao ulizikutanisha Azam FC na Mbao FC, kiukweli walihakikisha mashabiki wanakaa kwa kufuata umbali wa meta moja,”

“Pia waliweka maji na sabuni katika kila mlango na pia mashabiki wamekuwa wema kwani wanafuata kanuni zote tunazoelekeza kama zilivyotolewa na serikali,” alisema Nyambaya.

Nyambaya alisema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (TPBL) wamejipanga kuhakikisha mwongozo wa serikali kuhusu afya unatekelezwa ipasavyo siyo kwenye Ligi Kuu pekee hadi kwenye Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.

Nyambaya ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji alisema kituo cha Dar es Salaam kina Viwanja vya Taifa, Uhuru, Azam Complex na Meja Jenerali Isamuhyo, ambavyo vinatumika kwa Ligi Kuu, Daraja la Kwanza na Ligi Kuu ya Wanawake.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo, aliwashukuru mashabiki wote wa soka kwa Tanzania Bara kwa kuheshimu umbali wa meta moja katika michezo iliyochezwa Juni 13 na 14.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilianza kuendelea tena juzi baada ya kusimama tangu Machi 17 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19.

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi