loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ZFF yashauriwa tathmini ratiba ya ligi

SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF) limeshauriwa kuangalia upya utaratibu wa kuweka kituo kimoja kuchezwa Ligi Kuu, hasa katika suala zima la kuwaweka wachezaji kwa muda mrefu.

Katibu wa timu ya Chipukizi, Ali Juma Khamis alisema kuwa muda wa kukaa kambini kwa wachezaji wao utakuwa mkubwa, jambo ambalo litaweza kuwakosesha hata ajira zao kwa wale ambao wanafanya kazi katika sekta binafsi.

Alisema kuwa kwa mujibu wa ratiba alivyoiangalia timu itakaa kwa muda wa mwezi mmoja na siku kadhaa jambo ambalo kwa wachezaji wao, ambao wengi wao wamejiajiri na kuajiriwa katika sekta binafsi linakuwa ni kikwazo kwao.

Alifahamisha kwamba sio kama wanapingana na agizo la Serikali lakini ZFF ni bora wakarudi na kuzungumza na Serikali ili kuona suala hilo wanaliangalia vipi.

Hata hivyo, alisema kuwa bado anasikitika na kutopatiwa taarifa yoyote kama klabu za Pemba juu ya kinachoendelea na badala yake mambo mengi ambayo huamuliwa na shirikisho hilo huyapata kupitia vyombo vya habari.

Timu ya Chipukizi ni miongoni mwa timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar, ambapo hadi inasimama, timu hiyo ndio inayoshika mkia ikiwa na pointi tisa.

Kwa upande wake, Memeja wa klabu ya Jamhuri Abdalla Abeid ‘Elisha’ alisema kuwa hawaoni tatizo kumaliza ligi katika kituo kimoja, lakini tatizo ni kukaa kwa muda mrefu, hasa ikizingatiwa kuwa wachezaji pamoja na viongozi watashindwa kufanya kazi zao nyengine. hivyo Meneja huyo aliishauri ZFF kukaa kitako tena na kufikiria ratiba hiyo ili kuweka uwiyano sawa kwa klabu zote za Unguja na Pemba.

Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi wa Kamati ya Mashindano Ali Mohammed alisema kuwa suala la kulipa wachezaji ni jukumu la klabu na sio kwa shirikisho hilo wala Serikali.

Ligi Kuu ya Zanzibar itaendelea Juni 24 na tayari ratiba imeshatolewa, ambapo siku ya kwanza ya ligi hiyo jumla mechi nne zitachezwa mbili zikichezwa saa 8:00 mchana na mbili saa 10:00 zote zitachezwa katika viwanja vya Mao Dze Tong A na B.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo saa 8:00 mchana Selem View itacheza na Mafunzo Uwanja wa Mao A na Mau B kutakuwa na mchezo kati ya JKU na Mwenge, wakati saaa 10:00 Zimamoto itacheza na Mlandege katika Uwanja wa Mao A na KMKM na Jamhuri watacheza Mao B.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi