loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Eymael aweka sawa majeshi yake

HUENDA lile bao moja dhidi ya Azam FC, lilimuuma sana na sasa ameamua kuyaweka sawa majeshi yake kwa lengo la kulipiza kisasi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaofanyika kesho Uwanja wa Taifa.

Hiyo ni kauli ya kocha wa Yanga, Luc Eymael ambaye ameonesha nia ya dhati ya kutaka kuifunga Azam, baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa.

Jana Eymael aliliambia gazeti hili kuwa anawasoma wapinzani wake wote walioko mbele yake, hata hivyo kwa kufahamu kuwa Azam ni timu yenye wachezaji wazuri, lakini amepanga kutimiza azma hiyo ili kujiweka sawa kwenye nafasi za juu.

Aliwaheshimu wapinzani wake hao kwa kusema kuwa ni timu inayocheza mpira mzuri na wa kuvutia, vivyo hivyo timu yake inacheza mpira wa aina hiyo, alijipa imani na wachezaji wake kuwa watafanya makubwa zaidi katika siku ya Jumapili.

“Azam ni timu inayocheza soka safi, wana uzoefu na wachezaji wenye ubora, natarajia kuona aina ya mchezo mzuri kwa kuzingatia timu zote zinacheza soka la kuvutia lenye ushindani,” alisema Eymael.

Alisema wachezaji wake walicheza mchezo dhidi ya JKT Tanzania, ikiwa ni siku nne tu tangu ilipocheza na Mwadui FC, Pamoja na safari ya kurejea Dar es Salaam, ni wazi walikuwa katika uchovu.

Akiendelea kutoa ufafanuzi zaidi, alijipa matumaini ya wachezaji wake kurudi katika hali ya kawaida kwa kuwapa programu maalumu na kuwapa hamasa kwa namna ya kipekee huku akifahamu wazi kuwa watacheza na timu iliyopumzika zaidi yao.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa nafasi ya tatu na pointi 55, huku wapinzani wao Azam wakiwa nafasi ya pili na jumla ya pointi 57 wote wakiwa na michezo sawa.

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi