loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Riadha taifa sasa Septemba 5-6

SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT) limetangaza kuahirishwa kwa mashindano ya taifa yaliyopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa siku mbili kuanzia Agosti 15, imeelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na RT, mashindano hayo, ambayo hushirikisha mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, sasa yatafanyika kwenye uwanja huohuo kuanzia Septemba 5-6 mwaka huu.

Uamuzi huo wa kusogezwa mbele kwa mashindano hayo, umefikiwa katika kikao cha pamoja kati ya viongozi wa RT, Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Sababu za kuahirishwa kwa mashindano hayo, ni kutokana na nafasi ya malazi kwa washiriki kushindwa kupatikana kwa tarehe zilizopangwa awali yaani Agosti 15-16. RT imewaomba radhi wanachama wake, ambao ni mikoa kutokana na kuahirisha mashindano hayo, ambayo hayajafanyika kwa miaka mingi.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji wa RT, Tullo Chambo inaitaka mikoa kuendelea na mazoezi ili kuhakikisha wanaleta timu zenye ushindani katika mashindano hayo ya taifa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi