loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba raha tu

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba haikamatiki, baada ya jana kulipa kisasi kwa Mwadui FC kwa kuwafunga mabao 3-0, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yalifungwa na Hassan Dilunga, Augustino Samson aliyejifunga na John Bocco.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha ya pointi 75 na mabao ya kufunga 67 ikijiweka karibu na taji la ligi la tatu mfululizo; na kusubiri mechi tatu ili kutangazwa rasmi bingwa wa msimu wa 2019/20.

Kwa pointi hizo Azam FC inayoshika nafasi ya pili imeachwa kwa pointi 15 huku Yanga inayoshika nafasi ya tatu ikiachwa kwa pointi 20 ambazo ni ngumu kwa klabu hizo kuifikia Simba kwa haraka.

Simba waliingia uwanjani kwa kasi wakionesha uchu wa kutaka kumtafuna mtu mapema baada ya kusogea langoni mwa Mwadui mara kadhaa na hatimaye kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya tisa, Dilunga akitumbukiza wavuni mpira kufuatia pasi nzuri ya Bocco.

Kutokana na kasi ya mashambulizi langoni kwa Mwadui mchezaji wa Mwadui, Samson alijifunga dakika ya 21 baada ya kupokea krosi ya Shomari Kapombe. Kipindi cha kwanza kilimalizika Simba ikiwa mbele kwa mabao 2-0 ikiongoza pia, katika umiliki wa mpira.

Kipindi cha pili walirejea tena kwa kasi na kupata bao la tatu dakika ya 58 lililofungwa na Bocco kwa kichwa akimalizia mpira uliogonga mwamba uliopigwa na Luis Miquissone.

Simba walikuwa na uwezo wa kuondoka na mabao zaidi kama washambuliaji wake wangetulia kutokana na kupata nafasi kadhaa

kwa vipindi tofauti na kushindwa kufunga kutokana na kukosa umakini. Baadhi ya wachezaji waliokosa nafasi hizo adhimu ni Luis, Dilunga, Kapombe, Bocco na Kagere.

Mwadui ilishindwa kabisa kupenya langoni kwa Simba kutokana na safu ya ulinzi ya wapinzani wao kuwa makini na matokeo yake kuna kipindi walikuwa wanapoteza mpira kila walipokaribia ndani ya eneo la hatari.

Simba ilifanya mabadiliko kadhaa ikiwatoa Bocco, Luis, Dilunga, Kapombe, Gerson Fraga na kuingia Meddie Kagere, Clatous Chama, Francis Kahata, Yusufu Mlipili na Mzamiru Yassin lakini hawakuchangia lolote kwani hadi mpira unaisha mabao yalikuwa 3-0.

Mwadui pia ilifanya mabadiliko ingawa hayakuwasaidia. Iliwatoa Mussa Chambenga, Raphael Aloba na Ottu Joseph na kuingia Malik Jaffar, Abubakari Kambi na Enric Nkosi.

Kikosi cha Simba kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe/ Yusuph Mlipili (dk 73), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Kennedy Juma, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Gerson Fraga, Said Juma, John Bocco/ Meddie Kagere (dk 63), Luis Miquissone/ Clatous Chama (dk 63) na Hassan Dilunga/ Francis Kahata (dk 63).

Mwadui FC; Mahmoud Amour, Mfaume Omar, Yahya Mbegu, Joram Mgeveke, Augustino Simon, Frank John/ Mussa Chambenga (dk 56), Ottu Joseph, Enrick Nkhosi, Raphael Aloba/ Maliki Jaffary (dk 68), Gerlad Mdamu na Herman Masenga/ Omar Daga (dk 21).

Mechi nyingine zilizochezwa jana, KMC iliifunga Ruvu Shooting 2-1, Namungo iliifunga Kagera Sugar 2-0, Polisi Tanzania ilitoka sare ya 1-1 na Lipuli.

Coastal Union ilitoka suluhu na Mtibwa Sugar, Ndanda FC ikaitungua Biashara United bao 1-0, Mbeya City ikafungwa na Alliance 1-0 na JKT Tanzania ikazidi kuzamisha jahazi la Singida United kwa mabao 2-0.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi