loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

YANGA KUSAKA NAFASI YA PILI

BAADA ya tambo za hapa na pale leo Yanga na Azam FC, zitajitupa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Azam inashika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya wapinzani wao, kwa maana hiyo kama watapoteza mchezo huo Yanga itapanda nafasi ya pili na kama Azam itashinda basi itaendelea kubaki katika nafasi hiyo.

Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa katika mchezo wa raundi ya kwanza kwa bao 1-0 ambalo Ally Mtoni alijifunga na baadaye kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 79, baada ya kumkanyaga kwa makusudi beki Nicolaus Wadada.

Yanga imepania kuhakikisha inalipa kisasi kama alivyosema kocha wao Luc Eymael, akijinasibu wachezaji wake wako imara licha ya kukosa muda mwingi wa kupumzika.

“Wachezaji walikuwa na uchovu baada ya kucheza michezo miwili kwa muda mfupi ila wamefanya programu maalumu ya kuwaweka sawa, tutegemee mchezo wenye ushindani kwa pande zote mbili,” alisema Eymael.

Naye Ofisa habari wa Azam FC, Thabit Zakaria alitoa taarifa njema kwa mashabikiwa timu hiyo, kuwa wachezaji Never Tigere na Bruce Kangwa wamerejea nchini na tayari wameungana na timu hiyo.

“Tunawasubiri wengine watatu kutoka Ghana, Razak Abarola, Yakub Mohammed na Daniel Amoah ambao na wao taarifa za awali zilikuwa leo wafungue mipaka, kama hali ya janga la corona itakuwa nzuri wachukue ndege warejee,”alisema Zakazi.

Rekodi zinaonyesha tangu msimu wa 2015/2016, katika michezo 10, ya ligi kuu, Yanga imeshinda michezo minne, sare tatu na Azam imeshinda michezo mitatu tu.

Katika michezo minne ya mwisho Yanga imeshinda mara moja tu,iliyobaki Azam alifanikiwa kuondoka na ushindi, hata hivyo timu zote zimeonekana kuwa na soka la kuvutia msimu huu na kila mmoja kuweka mikakati yake.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi