loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TAVA kuendesha kozi ya wavu ufukweni

CHAMA cha mpira wa wavu Tanzania (TAVA) kinatarajia kuendesha mafunzo ya ukocha wa wavu ya ufukweni ngazi ya awali yatakayofanyika Juni 26 hadi 30, katika ufukwe wa Mbalamwezi, Dar es Salaam.

Akizungumza jana Katibu Mkuu wa TAVA, Alfred Selengia, mafunzo hayo yatawahusu walimu wa michezo mashuleni, vyuoni, makocha na wachezaji wa mpira wa wavu nchini.

“Tunawaalika makocha, wachezaji, walimu wa michezo mashuleni na vyuoni wenye malengo ya kujiendeleza katika fani ya ukocha.

Ada ya ushiriki ni Sh 35,000 na kila mshiriki atajigharamia usafiri, chakula na malazi,” alisema Selengia na kuongeza kuwa ushiriki uthibitishwe kabla ya Juni 24.

Alisema lengo ni kutambulisha wavu ya ufukweni shuleni ili ifikapo mwaka 2023 mchezo huu uwe unashindaniwa katika michezo ya shule za msingi na sekondari na Vyuoni (Umitashumta, Umisseta, Shimivuta na Tusa).

Pia Selengia amesisitiza mikoa kuendelea na ligi baada ya michezo kuruhusiwa kuendelea tena baada ya kusimama kwa zaidi ya miezi miwili baada ya janga la corona.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi