loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Minziro aomba ushirikiano Mbao FC

KOCHA mpya wa Mbao FC ya Mwanza, Fred Minziro amesema ili aweze kuibakisha timu hiyo kwenye mikono salama anahitaji kupewa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi na mashabiki.

Minziro ni miongoni mwa makocha wazawa wenye bahati ya kupandisha timu lakini mara inapopanda ligi kuu anatupiwa virago.

Mwaka jana Singida United ikiwa katika hali mbaya licha ya kuwa yeye ndiye aliyeipandisha na baadaye kutimuliwa alirudishwa tena kuinusuru isishuke daraja ns kufanikiwa kuibakisha.

Akizungumzia kibarua chake kipya, Minziro alisema uwezekano wa kuibakisha Mbao salama upo kama tu kutakuwa na ushirikiano kutoka kwa benchi la ufundi, wachezaji na viongozi.

“Tunaweza kuibakisha timu lakini ushirikiano na juhudi vinahitajika, nimeona baadhi ya mapungufu ni kufanyia kazi ili mambo yaweze kwenda sawa,” alisema.

Minziro alisema anataka kufanyia kazi safu ya ushambuliaji kuhakikisha inafanya vizuri pamoja na kurudisha uimara wa wachezaji waweze kupambana.

Baadhi ya makocha waliokuwepo kama Hemed Morocco na Abdulmutik Haji walishindwa kuendelea na sasa inatizamwa kama Minziro ataweza kuvumilia hali iliyopo na kuipandisha.

Kwa muda mrefu Mbao imekuwa haiko vizuri huku ikikabiliwa na ukata hali iliyosababisha kutajwa hivi karibuni kuwa wanataka kuuza timu ingawa baadaye ilikanushwa.

Timu hiyo inashika nafasi ya 19 ikiwa na pointi 23 katika michezo 30 hivyo, Minziro atakuwa ana kibarua kizito cha kuhakikisha anainusuru kutoka ilipo na kupanda juu.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi