loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mfaume kuwania mkanda wa IBA

BONDIA wa ngumi za kulipwa Mfaume Mfaume atakuwa wa kwanza barani Afrika kuweka historia ya kuchukua ubingwa wa kimataifa wa mabara (IBA) kama atashinda pambano lake dhidi ya Mfi lipino, Arnel Tinampay.

Pambano hilo la raundi 12 katika uzito wa kilo 70 limeandaliwa na promota Jay Msangi linatarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili Msangi alisema katika bara la Afrika hakuna bondia yeyote aliyewahi kuwania mkanda huo ambao makao yake makuu unatoka Marekani.

“Ni faraja kuona Mfaume Mfaume anapigania mkanda ambao umechezwa na mabondia mbalimbali duniani, katika bara ya Afrika hakuna yeyote aliyewahi ndio mara ya kwanza unatua Tanzania, akishinda ataweka historia mpya,”alisema.

Ujio wa Tinampay nchini hautakuwa mara ya kwanza kwani mwaka jana alichuana na Hassan Mwakinyo na kupigwa kwa pointi.

Msangi alitaja sababu za kumrejesha Tinampay nchini kuwa ni kwa vile staili yake inafanana na Mfaume lakini kingine anataka kuwatengeneza mabondia wengine katika hadhi ya kimataifa.

Alisema tayari amemalizana na mabondia wote wawili na wamesaini mkataba na anaendelea kufanya mazungumzo na wadhamini mbalimbali, baadaye atatangaza tarehe ya pambano lakinilitakuwa ndani ya mwezi Agosti mwaka huu.

Promota huyo alisema pambano hilo litasimamiwa na Wamarekaniwenye mkanda huo wa IBA huku akiamini kuwa Mfaume ana nafasi ya kufanya vizuri kwa sababu mitindo yao ya upigaji inafanana.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi