loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakazi atangaza nia Jimbo la Ukonga

MSANII wa muziki wa Hip Hop nchini Wabiro Wassira ‘Wakazi’ ametangaza nia ya kuwania ubunge kupitia Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza jana katika mkutano wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam jana Wakazi ambaye ni mwanachama wa chama cha ACT Wazalendo alisema amekuwa mwanaharakati wa muda mrefu wa masuala ya haki na usawa hivyo ameona ni wakati sasa wa kuwa kiongozi.

”Kwa sababu nimepata heshima ya kuitwa hapa mbele ya mkutano naomba nitumie nafasi hii kutangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika Jimbo langu la Ukonga,” alisema.

Hivi karibuni Wakazi alikabidhiwa kadi ya chama namba 0920827 ya hicho na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Baada ya kupokea kadi hiyo alisema

“Kwa sasa mimi ni mwanachama, nimependa sera na itikadi zake ambazo zitatupa maendeleo, baadaye kama chama kikinipa ridhaa nitakuwa kiongozi, kila kitu ni siasa, ni ngumu kama kijana kusema hafanyi siasa kwa sababu asilimia 70 ya Watanzania ni vijana na watoto,”.

Jimbo la Ukonga ni kama lipo wazi kwa sasa kwa sababu Mbunge anayemaliza muda wake, Mwita Waitara inadaiwa anataka kwenda kugombea nyumbani kwao mkoa wa Mara na nguvu nyingi amelekeza huko.

Endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge atakuwa msanii wa tatu kuingia bungeni, kuungana na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Mbunge wa Mbeya Mjini na Joseph Haule ‘ProfesaJay’ ambaye ni Mbunge wa Mikumi.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa adhabu ya kumfungia miaka ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi